Tuesday, October 27, 2015
MAWAZIRI WA JK WLIOANGUKA KWENYE NAFASI YA UBUNGE MWAKA HUU 2015
Do you like this story?
Mawaziri watano
wa Serikali inayomaliza muda wake wameanguka kwenye uchaguzi majimboni mwao,
sambamba na wagombea wengine maarufu wa Bunge lililopita baada ya matokeo ya
kura zilizopigwa Jumapili kuanza kutangazwa jana.
Mawaziri hao
wanaungana na wabunge wengine maarufu wa Bunge la Kumi walioshindwa kutetea
majimbo yao, wakiwamo wa kambi ya upinzani ambao wameangushwa na wagombea wa
CCM.
Pia wamo
mawaziri wa zamani wawili, Cyril Chami na Omary Nundu walioanguka kwenye
uchaguzi, kwa mujibu wa matokeo ambayo yanaendelea kutangazwa.
Tume ya Taifa
ya Uchaguzi (NEC) imesema jana kuwa itakamilisha kazi ya kutangaza matokeo yote
keshokutwa.
Mawaziri
walioanguka kwenye uchaguzi huo ni Steven Wasira, Christopher Chiza,
Aggrey Mwanri, Dk Steven Kebwe na Anne Kilango.
Katika matokeo
yaliyotangazwa jana, Wasira, kada maarufu na mwanasiasa mkongwe aliyekuwa
akitetea Jimbo la Bunda, alijikuta akiangushwa na mwanasiasa kijana, Ester
Bulaya, ambaye alihamia Chadema baada ya Bunge la Kumi kumaliza muda wake.
Wasira, ambaye
alikuwa Waziri wa Kilimo na Chakula, alianza mchakato wa uchaguzi mwaka huu kwa
kuomba ridhaa ya CCM agombea urais, lakini hakupitishwa. Bulaya, ambaye alikuwa
mbunge wa viti maalum (CCM), alipata kura 28, 508 na kumuacha mbali waziri huyo
mkongwe aliyepata kura 19, 126.
Mwingine
aliyeanguka ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu- Uwezeshaji na Uwekezaji,
Christopher Chiza ambaye ameangushwa na Bilago Samson wa Chadema katika Jimbo
la Buyungu. Waziri huyo alizidiwa kwa kura 104 baada ya Samson kupata kura
23,041 dhidi ya 22,934 za Chiza.
Lakini hali
haikuwa hivyo kwa Naibu Waziri wa Tamisemi, Aggrey Mwanri kwenye Jimbo la Siha.
Waziri huyo alizidiwa kwa zaidi ya kura 4,100 na mpinzani wake kutoka Chadema,
Dk Godwin Mollel aliyepata kura 22,746.
Katika Jimbo la
Serengeti, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Stephen Kebwe pia
alijikuta akipoteza nafasi ya kurudi bungeni kwa kura alipoangushwa na Marwa
Ryoba wa Chadema. Dk Kebwe alipata kura 39,232, akiwa amezidiwa na mpinzani
wake kwa zaidi ya kura 820.
Anne Kilango,
ambaye aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Elimu mwaka 2013 baada ya mabadiliko ya
Baraza la Mawaziri yaliyosababishwa na kashfa ya Operesheni Tokomeza,
ameangushwa na mgombea wa Chadema, Naghenjwa Kaboyoko wa Chadema kwa tofauti ya
kura 3,297.
Kilango alipata
kura 15,539 wakati mgombea huyo wa Chadema alipata kura 18,836. Pia wabunge
maarufu kama Vincent Nyerere (Musoma Mjini), James Lembeli (Kahama Mjini) na
Kyisieri Chambiri (Babati Mjini) wameangushwa.
Nyerere,
aliyekuwa akitetea kiti cha Musoma Mjini kwa tiketi ya Chadema, aliachwa mbali
na mgombea wa CCM, Vedastus Mathayo aliyepata kura 32, 836 dhidi ya 25,549.43
za Nyerere.
Lembeli, ambaye
alihamia Chadema muda mfupi baada ya Bunge la Kumi kumaliza muda wake, aliachwa
mbali na mfanyabiashara maarufu, Jumanne Kishimba aliyepata kura 47,553 dhidi
ya kura 30,122 za Lembeli.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAWAZIRI WA JK WLIOANGUKA KWENYE NAFASI YA UBUNGE MWAKA HUU 2015 ”
Post a Comment