Thursday, October 29, 2015

SUGU AZUNGUMZA JINSI CHADEMA ITAKAVYOFANYA KAZI MBEYA.




Mbunge mteule wa Jimbo la Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amesema chama hicho kitahakikisha kinampata meya mpya mwenye uwezo wa kusimamia miradi ya maendeleo inayopangwa kila mwaka.

Sugu aliyasema hayo jana, wakati akizungumzia mikakati ya Chadema baada ya kupata ushindi katika kata 26 kati ya 30 za jimbo lake.

“Tutamchagua meya atakayezuia mianya yote ya rushwa na uonevu pamoja na kusimamia sheria rafiki na siyo kandamizi,” alisema Sugu.

Alisema Mbeya itakuwa mfano wa kuigwa na majiji mengine ndani na nje ya nchi kutokana na mpangilio utakavyokuwa katika kutatua kero ambazo zilikuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo kwa wananchi.

Diwani mteule wa Kata ya Isanga, Anyandwile Mwalwiba, alisema wamejipanga kumpata meya atakayekuwa tayari kuendana na kasi kubwa ya maendeleo na kulibadilisha Jiji la Mbeya.

 

0 Responses to “SUGU AZUNGUMZA JINSI CHADEMA ITAKAVYOFANYA KAZI MBEYA.”

Post a Comment

More to Read