Monday, October 12, 2015
UTURUKI YAOMBOLEZA VIFO TAKRIBANI 95
Do you like this story?
Maelfu ya Watu wamekusanyika mjini Ankara
nchini Uturuki kuomboleza kwa ajili ya Watu takriban 95 waliouawa kwa milipuko
miwili ya mabomu.
Watu wanaounga mkono Chama cha Kikurdi ambao
walikuwepo kwenye mkutano katika eneo ambalo mabomu yalilipuka wanaamini kuwa
idadi ya kweli ya waliopoteza maisha ni Watu 128.
Vyanzo vya ulinzi vinasema kuwa vinashuku
kundi la wanamgambo wa IS kuhusika kwenye shambulio hilo.
Serikali imekana vikali madai kuwa imehusika
katika mashambulizi hayo.
Milipuko ya mabomu ilitokea karibu na kituo
cha treni cha mjini Ankara wakati watu walipokusanyika kwa ajili ya matembezi
yaliyoandaliwa na makundi ya mrengo wa kushoto yakishinikiza kukoma kwa
mapigano kati ya Serikali ya Uturuki na wanamgambo wa kikurdi.
Katika hali iliyotarajiwa, wanamgambo wa PKK
walitangaza kuweka silaha chini siku ya jumamosi, wakitoa wito kwa wapiganaji
wake kuachana na mapigano ya msituni nchini Uturuki , isipokuwa ikiwa ni kwa
ajili ya kujilinda.
Hata hivyo,siku ya jumapili Jeshi la nchi
hiyo lilisema limefanya mashambulizi ya anga dhidi ya wanamgambo hao,
likishambulia kusini mashariki mwa Utturuki na katika ngome za PKK kaskazini
mwa Iraq na kuua watu 49.
BBC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)


0 Responses to “ UTURUKI YAOMBOLEZA VIFO TAKRIBANI 95”
Post a Comment