Sunday, November 1, 2015
KAULI YA PROF JAY KWA WANAMIKUMI
Do you like this story?
Mbunge mteule wa jimbo la Mikumi kwa tiketi ya Chadema
Josephu Haule maarufu kama Profesa J amewashukuru wananachi wa jimbo hilo kwa
kumpa ridhaa na kuahidi kushirikiana na wananchi wote katika kuleta maendeleo
ya jimbo la Mikumi.
Akizungumza na wananchi wa jimbo la Mikumi mbunge huyo mteule
Profesa J amesema jimbo la Mikumi lilisahaulika kwa miaka mingi huku wananchi
wakiendelea kukosa huduma bora za kijamii ambapo amaesema atahakikisha
anaisimamia rasilimali za jimbo la Mikumi ziwanufaishe wananchi wote.
Kwingineko katika jimbo la Morogoro mjini viongozi wa vyama
vya upinzani wameeleza kutoridhishwa na matokeo ya uchaguzi wa madiwani katika
kata za Chamwino na mazimbu kutokana na uchaguzi wa kata hizo kugubikwa na
changamoto lukuki zikiwemo kuzalishwa vituo feki vya kupigia kura siku ya
uchaguzi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KAULI YA PROF JAY KWA WANAMIKUMI”
Post a Comment