Thursday, November 5, 2015
MAWAZIRI WAAGIZWA KUREJESHA IKULU MAGARI YA SERIKALI LEO
Do you like this story?
Katibu
Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue, amewaagiza Mawaziri na Naibu Mawaziri leo
kurudisha magari ya serikali baada ya Rais Mteule, Dk. John Magufuli kuapishwa
kwa kuwa ndiyo siku yao ya ukomo wa uongozi.
Akizungumza kwa
njia ya simu, Balozi Sefue alisema baada ya Bendera ya Rais kuteremshwa na
kabla Bendera ya Rais mpya kupandishwa, magari ya mawaziri na Naibu Mawaziri,
yatabadilishwa namba kwa kuondoa herufi ya cheo chake (W au NW) na kurejeshwa
kwenye namba za serikali (ST).
Balozi Sefue
alisema baada ya shughuli hiyo, magari hayo yatawarudisha nyumbani mawaziri na
naibu Mawaziri waliomaliza muda wao na kurejeshwa Ikulu tayari kwa ajili ya
kupewa mawaziri wapya watakaoteuliwa.
CHANZO:
NIPASHE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAWAZIRI WAAGIZWA KUREJESHA IKULU MAGARI YA SERIKALI LEO”
Post a Comment