Monday, November 2, 2015
NYALANDU APONGEZA ASKARI KWA KUMNASA JANGILI SUGU
Do you like this story?
JITIHADA
za serikali kwenye mapambano dhidi ya ujangili zinaendelea kuzaa matunda baada
ya Kikosi cha Kupambana na Ujangili kumkamata mtuhumiwa mkuu wa ujangili
anayejulikana kama Shetani.
Kukamatwa
kwa jangili huyo kumetokana na jitihada za usiku na mchana zilizofanywa kwa
ushirikiano wa Wizara ya Maliasili na Utalii na wadau wengine hususan askari wa
wanyamapori kwa kipindi cha mwaka mmoja kwenye maeneo mbalimbali ya uhifadhi
nchini.
Akizungumza
na UHURU wakati akielekea jijini London, Uingereza kwa safari ya siku mbili ya
kikazi, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, alisema kazi
iliyofanyika ni kubwa na inastahili pongezi.
Alisema
majangili wamekuwa wakiisumbua serikali kwa kipindi kirefu lakini kutokana na
jitihada za serikali na wadau wengine zikiwemo nchi wahisani wa maendeleo na
jumuia za kimataifa hali inaendelea kuwa nzuri.
Alisema
Shetani anakuwa wa pili kukamatwa baada ya Queen of Victory aliyekamatwa na
serikali kipindi cha nyuma akiendelea na jitihada za kufanya uhalifu wa kuua na
kuiba viungo vya wanyamapori wa Tanzania.
Waziri
Nyalandu alisema serikali itaendelea na mapambano ya kuwasaka na kuwachukulia
hatua za kisheria vigogo wa ujangili na wanaowasaidia kufanikisha uhalifu huo
hapa nchini.
Alisema
akiwa jijini London atahudhuria mkutano wa Mawaziri wa Utalii kutoka nchi
mbalimbali zikiwemo za Afrika Mashariki, ambao watazungumza mambo mbalimbali
yanayohusu namna za kuendeleza sekta ya Utalii katika ukanda wa Afrika
Mashariki.
Alisema
pia mkutano huo utahudhuriwa na Mwanahabari maarufu wa Shirika la Habari la CNN,
Richard Quest atakayefanya mahojiano maalumu kuhusu masuala ya Utalii na
Maliasili.
Kuhusu
hali ya siasa nchini, Nyalandu alisema uchaguzi umeisha na kwamba
viongozi walioshinda wanapaswa kufahamu kuwa si wao walioshinda bali ni
watanzania kwa ujumla hivyo wawe wamoja kuijenga Tanzania.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ NYALANDU APONGEZA ASKARI KWA KUMNASA JANGILI SUGU”
Post a Comment