Monday, November 2, 2015
WAKAZI WA JIJI LA MWANZA WATAABIKA NA MAFURIKO KUTOKANA NA MVUA INAYOENDELEA KUNYESHA
Do you like this story?
![]() |
Maji hadi ndani, hakika ni hatari |
Miongoni mwa nyumba zilizopo Mtaa wa Kilimahewa Manispaa ya Ilemela
Mkoani Mwanza ambazo huathirika na kero ya Maji kuingia ndani pindi mvua
zinapoanza kunyesha.
Pichani ni mmoja wa wakazi wa Kilimahewa akitoa maji ndani ya nyumba yake
kutokana na mvua iliyoanza kunyesha majira ya saa kumi na mbili alfajiri hii
leo. Hadi tunaenda hewani (saa 10:30 asubuhi) Mvua hiyo inaendelea kumiminika
mdogomdogo.
Picha na Loyce Nhaluke
Mbali na Kilimahewa, Pia wakazi wa Mabatini Jijini Mwanza hukumbwa na
kero ya Mafuriko wakati wa Mafuriko na kwa miaka mingi juhudi za kuwahamisha
zimekuwa zikigonga mwamba linapokuja suala la kuwatafutia makazi mapya.
Mara kadhaa mafuriko katika maeneo hayo yamekuwa yakisababisha athari
mbalimbali ikiwemo vifo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WAKAZI WA JIJI LA MWANZA WATAABIKA NA MAFURIKO KUTOKANA NA MVUA INAYOENDELEA KUNYESHA”
Post a Comment