Wednesday, November 4, 2015
UFAFANUZI WA TUKIO LA KUANGUKA KWA JUKWAA LA JENGO LA NHFI MKOANI MBEYA
Do you like this story?
Mwonekano wa jengo la mfuko huo linalojengwa mkoani Mbeya. |
![]() |
Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti akifafanua
jambo wakati akizungumza waandishi wa habari kuhusu kuvunjika kwa uzio wa
jengo la mfuko huo linalojengwa mkoani Mbeya.
|
Utangulizi:
Moja ya
mikoa ambayo inaendelea na ujenzi huo ni Mbeya, ambako Mfuko unajenga jengo la
ghorofa kumi na mbili litakalokuwa na nafasi za ofisi na huduma nyingine ndani
yake.
Tukio
la Kuanguka kwa jukwaa:
Wakati
shughuli hizo za ujenzi zinaendelea, jana mchana katika hali isiyotarajiwa mvua
iliyoambatana na upepo mkali ilinyesha mjini Mbeya. Upepo na mvua hizo
vilisababisha kuanguka kwa jukwaa la jengo hilo na kutua juu la paa la jengo la
ofisi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani Mbeya. Kuanguka kwa jukwaa
hilo hakukuwa na madhara yoyote kwa maisha ya binadamu, kwa maana kuwa hakuna
mtu aliyepoteza maisha au kupata majeraha. Hata hivyo tukio hilo lilisababisha
taharuki kwa wafanyakazi wapatao hamsini waliokuwemo ndani ya jengo hilo na
hivyo kusababisha kazi kusimama kwa muda. Aidha tathmini ya awali iliyofanyika
katika paa la jengo la TANESCO lililoangukiwa na jukwaa hilo inaonyesha kuwa
paa hilo ilipata hitilafu ndogo ambayo itafanyiwa marekebisho kwa gharama za
Mkandarasi anayejenga jengo la NHIF.
Hatua
za kisualama zilizochukuliwa:
Kama
sheria za ujenzi zinavyoagiza, kabla ya kuanza kwa ujenzi wa jengo hilo
Mkandarasi alishajenga uzio kuzunguka jengo zima ili kuhakikisha kuwa shughuli
za ujenzi hazileti madhara kwa wapita njia au ofisi zilizo jirani. Umakini wa
Mkandarasi huyo katika kuzingatia taratibu za tahadhari katika shughuli za
ujenzi, umewezesha jengo hilo la ghorofa kumi na mbili kufikia hatua nzuri ya
ujenzi bila madhara yoyote kwa wajenzi wenyewe, wapita njia au ofisi za jirani.
Aidha
kufuatia tukio la Jumatatu 02/11/2015, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
umeshamwandikia Mkandarasi anayeendelea na ujenzi katika jengo hilo kuhakikisha
kuwa uzio unaozunguka jengo zima unaimarishwa zaidi hususani wakati huu
tunapokaribia kipindi cha mvua za masika ili kuepuka uwezekano wa madhara
yoyote kwa binadamu wakati shughuli za ujenzi zinaendelea.
Namna
Habari ilivyoripotiwa:
Tunapenda
kuufahamisha umma kwamba habari zilizoripotiwa jana na baadhi ya vyombo vya
habari kwamba jengo la NHIF mkoani Mbeya limeporomoka, zilipotosha ukweli wa
tukio hilo, kwani kilichoporomoka siyo jengo, bali ni jukwaa.
Tunapenda
kusisitiza kuwa tukio hilo limesabishwa na mvua kubwa na upepo uliovuma katika
mji wa Mbeya, wala siyo uzembe wa Mkandarasi anayejenga jengo hilo.
Wito
kwa Wanachama wa NHIF:
Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya unawaomba wanachama na wadau wake nchini kote
waendelee kuwa watulivu na kuvuta subira kwani changamoto ya ufinyu wa ofisi
katika mikoa itakuwa imepatwa ufumbuzi baada ya kukamilika kwa ujenzi wa
majengo ya unaoendelea hivi sasa katika mikoa mbali mbali nchini.
Imetolewa
na:
Mkurugenzi
Mkuu,
Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “UFAFANUZI WA TUKIO LA KUANGUKA KWA JUKWAA LA JENGO LA NHFI MKOANI MBEYA ”
Post a Comment