Saturday, December 19, 2015
RAIS MAGUFULI AMTUMIA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE
Do you like this story?
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi
Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye amepatwa na
msiba mzito wa kufiwa na Dada yake Mpendwa Bi. Tausi Khalfan Kikwete kilichotokea
jana tarehe 17 Desemba, 2015 huko nchini India.
Katika salamu
hizo, Rais Magufuli amesema anaungana na familia ya Rais Mstaafu Kikwete katika
kipindi hiki kigumu cha majonzi ya kuondokewa na mtu muhimu kwa familia.
“Kwa masikitiko
makubwa nakupa pole nyingi Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete kwa
kufiwa na dada yako ambaye alikua nguzo muhimu katika familia” Amesema Rais
Magufuli.
Aidha Rais
Magufuli amemuomba Rais Mstaafu Kikwete kumfikishia salamu nyingi za pole kwa
familia nzima na amewaomba wawe na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi
hiki kigumu.
Rais Magufuli
amemuomba Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema aipumzishe roho ya marehemu Tausi
Khalfan Kikwete mahali pema peponi, Amina.
Imetolewa na;
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
18 Desemba,
2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)


0 Responses to “ RAIS MAGUFULI AMTUMIA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ”
Post a Comment