Monday, January 25, 2016
DIEGO COSTA AWAACHIA KILIO MASHABIKI WA ARSENAL KATIKA UWANJA WAO WA NYUMBANI, EMIRATES
Do you like this story?
Diego Costa akishangilia ushindi. |
Diego Costa (blue) akimtoka beki wa Arsenal, Hectoe Bellerin (nyekundu) katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza kati ya Arsenal na Chelsea. |
Refa wa mchezo huo, Mark Clattenburg akimwonesha Mertesacker kadi nyekundu. |
Mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa ameisaidia klabu yake kuibuka na
ushindi wa goli moja kwa bila mbele ya wapinzani wao wa kutokea jiji moja la
London, Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza, mchezo uliochezwa
katika uwanja wa Emirates unaomilikiwa na Arsenal.
Costa alifunga goli hilo katika dakika ya 23 baada ya kuunganisha mpira
mrefu uliopigwa na beki wa klabu hiyo, Branislov Ivanovic goli lilidumu kwa
dakika zote 90 za mchezo huo hadi mwamuzi Mark Clattenburg anapuliza filimbi ya
kumalizika kwa mchezo huo.
Aidha Arsenal ilimaliza mchezo huo ikiwa na wachezaji 10 pekee uwanjani
baada ya beki wa timu hiyo, Per Mertesacker kuonyeshwa kadi nyekundu katika
dakika 18 ya mchezo huo baada ya kumchezea vibaya mshambuliaji wa Chelsea,
Diego Costa.
Baada ya matokeo hayo Arsenal imebaki na alama zake 44 huku ikiwa katika
nafasi ya 3 nyuma ya Manchester Citty na Leister City na Chelsea ikipanda kwa
nafasi moja kutoka nafas ya 14 hadi 13 huku ikiwa na alama 28.
Matokeo mengine ya Ligi Kuu ya Uingereza iliyochezwa jana Jumapili,
Januari 24 ni Everton iliyowakaribisha Swansea City na mchezo huo kumalizika
kwa Swansea kuibuka na ushindi wa goli mbili kwa moja, magoli ya Swansea
yakifungwa na Gylfi Sigurdsson dakika ya 17 na Andre Ayew katika dakika ya 34
huku beki wa Swansea Jack Cork akijifunga goli la kufutia machozi kwa Everton
katika dakika ya 26.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “DIEGO COSTA AWAACHIA KILIO MASHABIKI WA ARSENAL KATIKA UWANJA WAO WA NYUMBANI, EMIRATES”
Post a Comment