Friday, January 22, 2016
HII NI STORY MPYA KUHUSU MANCHESTER UNITED NA PEP GUADIOLA
Do you like this story?
Manchester United wamekanusha kwamba
walikutana na boss wa Bayern Munich Pep Guardiola kuhusu uwezekano wa kuchukua
mikoba ya bosi sasa Louis van Gaal, baada ya soka Ufaransa kusema kuwa mkutano
ulifanyika jana mjini Paris, lakini United wamesisitiza kuwa hadithi hizo sio
za kweli.
Guardiola, 45, ataondoka Bayern Munich mwisho
wa msimu huu huku akisema kuwa anataka kufundisha soka nchini England.
Manchester City ndio wanaopewa kipaumbele
kumnasa Mhispania huyo, lakini Chelsea na Manchester United wao pia wamekuwa
wakihusishwa pamoja na kutaka kupata huduma ya bosi huyo.
Bayern Munich wapo katika kambi ya mafunzo
mjini Doha katika mapumziko ya baridi huku ligi kuu nchini Ujerumani
ikitarajiwa kurudi tena wikend hii ambapo Bayern Munich watacheza mchezo wao
dhidi ya Hamburg siku ya Ijumaa.
Guardiola, ambaye mkataba wake na Bayern
unafikia tamati katika majira ya joto, hapo awali alisema ana nia ya kufundisha
soka nchini England, hali iliyosababisha presha kubwa kwa makocha wa timu za
City na United ambao timu zao hazina muelekeo mzuri sana katika ligi.
Tayari Pep Guadiola amewaomba radhi makocha
nchini England kama kauli zake za kutamka kutaka kufundisha soka nchini England
zimesababisha presha miongoni mwao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “HII NI STORY MPYA KUHUSU MANCHESTER UNITED NA PEP GUADIOLA”
Post a Comment