Friday, January 22, 2016
TAMBWE APEWA MPIRA WA ‘KICHINA’
Do you like this story?
Amisi Tambwe akikabidhiwa mpira ambao haukuwa miongoni mwa ile iliyotumika kwenye mchezo wa Yanga vs Majimaji baada ya mschezaji huyo kufunga magoli matatu kwenye mechi hiyo |
Huu ndiyo mpira aliopewa Tambwe kwenye mchezo wa Yanga vs Majimaji baada ya kupiga hat-trick, mpira huu si miongoni mwa mipira inayochezewa kwenye ligi msimu huu |
Katika hali isiyo ya kawaida mshambuliaji wa
Yanga Amisi Tambwe jana alipewa mpira feki na mwamuzi John Fannuel
aliyechezesha mchezo wa jana (January 21, 2016) kati ya Yanga dhidi ya Majimaji
kwenye uwanja wa taifa, Dar es Salaam.
Tambwe alifunga magoli matatu kwenye mchezo
huo ambao Yanga walipata ushindi wa mago 5-0 dhidi ya Majimaji. Kwa mujibu wa
kanuni za soka, mchezaji anayefunga magoli zaidi ya mawili hupewa mpira mmoja
kati ya ile ambayo ilitumika kwenye mchezo husika.
Lakini jana mambo yalikuwa tofauti, wakati
mwamuzi wa mchezo huo anamkabidhi Tambwe mpira wake, mshambuliaji huyo
alishtuka kwamba mpira aliopewa haukuwa miongoni mwa ile iliyotumika kwenye
mchezo wao dhidi ya Majimaji. Alipodai mpira uliotumika kuchezea mchezo husika
mwamuzi alitia ngumu.
Baada ya kugundua ujanja huo uliofanywa na
mwamuzi, mtandao huu ulimfuata mwamuzi huyo na kumuuliza kwanini Tambwe
hakukabidhiwa mpira uliotumika kwenye mechi ya Yanga na Majimaji? Mwamuzi huyo
alisema huo ndiyo utaratibu uliopo na kama kuna maswali zaidi basi waulizwe
wasimamizi wa ligi.
Mbali na hayo, Tambwe alisema hat trick yake
inamwendea moja kwa moja mchumba wake. Hat-trick hiyo ni ya pili kwa Tambwe
msimu huu, nyota huyo alipiga bao tatu kwa mara kwanza kwenye msimu huu
December 19, 2015 wakati Yanga ilipocheza na Stand United na ku-dedicate bao
hizo tatu kwa mtoto wake.
Kwenye mchezo kati ya Yanga dhidi ya Stand
United Tambwe alikabidhiwa mpira uliotumika kwenye mchezo huzika lakini cha
kushangaza ni mpira aliopewa jana ambao haukuwa miongoni mwa ile inayotumiwa
kwenye ligi msimu huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ TAMBWE APEWA MPIRA WA ‘KICHINA’”
Post a Comment