Friday, January 22, 2016

MKUU WA MKOA WA MBEYA ABBAS KANDORO AKEMEA WAVAMIZI WA VYANZO VYA MAJI.


Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mh Nyilembe Munasa akiwa anapanda Mti kwenye chanzo cha maji cha Mto imeta kilichopo katiaka Hifadhi ya Msitu wa safu za Mlima Mbeya katika kata ya Iganzo(.Picha na David Nyembe wa Fahari News)

Wananchi wakiwa wanapanda Miti katika maeneo ya Mlima Mbeya(.Picha na David Nyembe wa Fahari News)


Wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira wakiwa wanabeba miti Tayari kwa kwenda kupanda.(.Picha na David Nyembe wa Fahari News)

Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Bw Samweli Lazaro akiwa anapanda Mti.(.Picha na David Nyembe wa Fahari News)


Mzee nae akuwa Nyuma kwenye zoezi la upandaji Miti

Watumishi wa Almashauri ya Jiji wakiwa wapepunzika mara baada ya kumaliza kupanda Miti.(.Picha na David Nyembe wa Fahari News)

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyilembe Munasa(Kushoto) Osea Cheyo(katikati)na Kaimu Mkurugenzi wa jiji la mbeya Bw Samweli Lazaro wakiwa kwenye Picha ya pamoja mara baada ya kumaliza zaoezi la upandaji  Miti.(.Picha na David Nyembe wa Fahari News)


Mkuu wa mkoa Mbeya ndugu Abbas Kandoro ameziagiza halmashauri zote za wilaya katika mkoa wa mbeya na hifadhi za taifa zote kuwaondoa watu wote waliovamia maeneo ya hifadhi za misitu pamoja na hifadhi ya misitu mlima Mbeya, na wale wanaofanya shughuli za kibinadamu kando kando ya mito kuacha kufanya hivyo mara moja ambapo ametoa siku 14 kwa halmashauri zote kufanya tathmini na kutekeleza agizo hili.

Agizo lilitolewa katika hotuba iliyosomwa na  mkuu wa wilaya ndg. Nyirembe Munasa ambae alimuwakilisha mkuu wa mkoa katika uzinduzi wa wa kampeni ya upandaji miti hapo jana ambapo kimkoa lilifanyika katika chanzo cha maji mto  Imeta kilichopo kata ya Iganzo, ambapo jumla ya miti elfu kumi  na sita ilipandwa ikiwemo miti ya kuhifadhi vyanzo vya maji elfu kumi na tano (15,000) na miti ya kivuli na matunda elfu moja (1,000)

Katika hotuba hiyo Munasa aliwaasa wananchi kutunza miti iliyokwisha pandwa kwa kuikinga na moto pamoja na kurudishia ile ambayo imekufa na kwamba ni kazi bure kuendelea kupanda miti wakati ile iliyopandwa msimu  uliopita ikiachwa bila matunzo hivyo aliwataka wanachi pamoja na viongozi katika ngazi mbali mbali kufanya tathmini ya miti iliyopandwa mwaka jana na kuhakikisha wanairudishia miti yote ambayo imekufa na kuendelea kuitunza vema ile ambayo inaendelea vizuri

Hata hivo Munasa aliwasisitiza wananchi kudumisha mila, desturi na tamaduni nzuri zinazolenga kuamsha ari ya upandaji, utunzaji miti na kuchochea uendelezaji na uhifadhi wa mazingira yanayowazunguka ili kuleta mabadiliko ya kimaendeleo na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi yaliyo anza kuleta athari katika maeneo mengi na kwamba serikali imeweka lengo la kupanda miti isiyopungua milioni moja na nusu kwa mwaka katika kila halmashauri huku zoezi hilo likitarajiwa kukamilika na kufanyiwa tahtmini ifikapo mwezi Juni,

Aidha alihitimisha hotuba kwa kuwataka wananchi kuyatunza maziringa na kuhakikisha wanafuata sheria na taratizu zote zinazohusiana na uhifadhi wa vyanzo vya maji na mazingira ambapo kauli mbiu mwaka huu ni “Panda Miti Kuhifadhi Vyanzo Vya Maji na Mazingira,”

0 Responses to “MKUU WA MKOA WA MBEYA ABBAS KANDORO AKEMEA WAVAMIZI WA VYANZO VYA MAJI.”

Post a Comment

More to Read