Thursday, January 7, 2016
WAFANYABIASHARA WAHIMIZWA KULIPA KODI KWA HIARI JIJINI MBEYA.
Do you like this story?
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Dk Samweli Lazaro akizungumza na waandishi wa Habari Ofini kwake.(.Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Waandishi wa Habari wakimsikiliza kwa makini Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya.(.Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Wakuu wa Idara Mbalimbali wa Almashauri ya jiji la Mbeya(.Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Halmashauri ya
jiji la Mbeya kupitia mkurugenzi wake dkt. Samwel Lazaro imewataka
wafanyabiashara wote wa jijini hapa kutoa kodi, tozo na ushuru wanaopaswa kutoa
ili kuiwezesha mamlaka ya halmashauri ya jiji kufanya kazi zake za kuwatumikia
wananchi ipasavyo.
Mkurugenzi wa
jiji amesema kuwa ili halmashauri iweze kutoa huduma za kijamii ipasavyo, basi
ni vema wafanyabiashara wakaacha kukwepa kodi wanazopaswa kuzitoa. Halmashauri
ya jiji la Mbeya imefanikiwa kukusanya kiasi cha 24% pekee mpaka kufikia mwezi
novemba kwaka 2015, 74% pungufu ya makadirio ya ukusanywaji wa mapato kwa mwaka
wa fedha 2015-2016.
Akieleza mbele
ya waandishi wa habari dkt. Lazaro amesema kuwa kati ya sababu kuu
zilizosababisha upatikanaji wa mapato kwa kiasi hicho kidogo ni pamoja na ukwepaji
kodi uliokithiri kwa wafanya biashara na kuongeza kuwa kiasi cha mapato
yanayopatikana ndio kiasi cha utekelezwaji wa huduma za jamii zinazofikishwa
kwa wananchi hivyo ili huduma za jamii ziwe timilifu lazima mapato yakusanywe
ipasavyo kutoka katika vyanzo ikiwamo ushuru, tozo na kodi kutoka kwa wafanya
biashara wakubwa na wadogo.
Pamoja na hayo, Mkurugenzi wa halmashauri ya
jiji la Mbeya amesema kuwa serikali imeidhinisha kiasi cha shilingi za
kitanzania bilioni 12 kwaajili ya uboreshaji wa miundombinu katika jiji la
Mbeya ikiwa ni pamoja na uwekwaji wa taa za barabarani, ujenzi wa mifereji
katika barabara, ujenzi wa njia za kuelekea katika makazi ya watu (access
roads), ujenzi wa maghuba makuu mawili ya taka n.k ambapo hii ni katika
barabara zote mpya zilizojengwa na halmashauri ya jiji la Mbeya ambazo
zinaurefu wa km 23.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WAFANYABIASHARA WAHIMIZWA KULIPA KODI KWA HIARI JIJINI MBEYA.”
Post a Comment