Saturday, January 9, 2016
WAHAMIAJI HARAMU 79 WAMEKAMATWA KWA KUISHI NCHINI BILA KIBALI MAALUMU NA KUSABABISHA KUKOSEKANA KWA AJIRA KWA WATANZANIA KWA WAO KUFANYA HIZO KAZI
Do you like this story?
Raia wa kigeni 79 wamekamatwa na Idara ya Uhamiaji
nchini kwa kosa la kuishi nchini bila vibali na kufanya kazi wasizo na taaluma
nazo.
Naibu Kamishna wa Uhamiaji Dar es Salaam, John
Msumule jana alisema watuhumiwa hao wanatoka katika nchi 15.
Nchi hizo na idadi ya wahamiaji haramu ni Nigeria
(4), China (20), Ethiopia (23), Korea (9), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC
(6), Somalia (3),Uganda (2), Madagascar (5), Burundi (2), Ivory Coast (1), Lebanon
(1), India (1), Zimbabwe (1) na Ghana (1).
Alisema katika ‘kamata kamata’ hiyo pia wamefanikiwa
kukamata Watanzania watatu, ambao wamekuwa wakijishughulisha na kukusanya,
kuwahifadhi na kuwasafirisha wasichana kuwapeleka nchi za mbali, kwa ajili ya
kufanya kazi mbalimbali.
“Tumewakamata wasichana sita ambao walikuwa
wamekusanywa na watanzania hao ili kusafirishwa na tutawachukulia hatua za
kisheria ili kutoa fundisho kwa wengine wenye nia ya kufanya mtindo kama
huu,”alisema Msumule.
Aliongeza kuwa idara hiyo imewarudisha nchini mwao
wahamiaji 23 raia wa Ethiopia na watuhumiwa nane wa nchi
mbalimbali,wamefikishwa mahakamani. Alisema shughuli ya kuwarejesha raia
wengine katika nchi zao zinaendelea.
Msumule aliwataka wamiliki wa nyumba za kulala wageni
na nyumba za kupanga, wahakikishe wanatambua wateja wao ni raia wa wapi na
anafanya kazi gani, kabla ya kufanya naye mkataba wa aina yoyote.
Aliwataka pia watanzania wanaooa na kuolewa,
wahakikishe wanafahamiana na mtu huyo na kumchunguza kujua anakotoka na yupo
nchini kwa kazi gani, la sivyo mtu akibainika anaishi na mhamiaji, anaweza
kujiingiza katika matatizo.
“Sisi hatutajali, tutamkamata kwa kosa la kumhifadhi
kwa hiyo lazima wajenge dhana ya kuwachunguza watu hao, hata wasichana wa kazi
za ndani, lazima umjue vizuri na sio unamchukua tu bila kujua historia yake
,” alisema.
Msumule aliwataka raia wengine ambao hawana vibali
vya kuishi nchini, waondoke wenyewe na wasisubiri hadi sheria ichukue mkondo
wake.
“Wapo wengi, tunachoomba waondoke wenyewe bila kushurutishwa,wengine
wanafanya kazi ambazo hata watanzania wanaweza kuzifanya, wakubali na
waondoke,” aliagiza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WAHAMIAJI HARAMU 79 WAMEKAMATWA KWA KUISHI NCHINI BILA KIBALI MAALUMU NA KUSABABISHA KUKOSEKANA KWA AJIRA KWA WATANZANIA KWA WAO KUFANYA HIZO KAZI ”
Post a Comment