Monday, February 1, 2016
BUNGE LATENGUA KANUNI KUJADILI MPANGO WA SERIKALI
Do you like this story?
Akitengua kanuni Waziri wa Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Walemavu katika Serikali ya Awamu ya Tano, Jenista Mhagama
amesema kwamba bunge lilitakiwa likae kama kamati mwezi Nombemba ili liweze
kujadili mpango wa serikali lakini kutokana na uchaguzi mkuu uliokuwepo nchini
kazi hiyo ilishindikana.
Kwa msingi huo kutokana na uwezo wa bunge
kupitia ibara ya 63 (3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
inayowezesha bunge kujadili mipango ya serikali,kwa muda muafaka serikali
imeamua kutengua kanuni ili bunge likae kama kamati kwa muda wa siku 5 ili
kujadili mpango wa serikali ili wabunge waweze kuishauri serikali kabla ya
bunge la bajeti.
Aidha mpango huo ulishindwa kujadiliwa
bungeni hapo juzi kutokana na kanuni za bunge kukiukwa kwa kusomwa bila
kutengua kanuni ya 94(1).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ BUNGE LATENGUA KANUNI KUJADILI MPANGO WA SERIKALI”
Post a Comment