Monday, February 1, 2016
SIMBA YAZINDUA DUKA LA VIFAA VYA MICHEZO
Do you like this story?
Rais wa klabu ya Simba (katikati) akikata utepe kuzindua duka la kuuza vifaa vya Simba lililopo Dar Free Market Mall Ground Floor |
Katika kukuza wigo wake wa mapato pamoja na
upatikanaji wa vifaa, klabu ya Simba leo imezindua duka lake rasmi kwa ajili ya
kuuza vifaa vya michezo vyenye chapa ya Simba.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Rais wa Simba
Evans Aveva alisema “kama mtakumbuka
moja ya malengo ambayo uongozi wangu huu uliopo madarakani ulijiwekea ni pamoja
na kuongeza wigo wa mapato kupitia vyanzo vyake vilivyopo lakini pia kuja na
mkakati kabambe kwa ajili ya kuongeza na leo wote tunakuwa mashuhuda katika
kuzindua duka letu la vifaa vya michezo.
Duka ambalo litakuwa likiuza kila
bidhaa ambayo inachapa Simba hivyo wanachama na wapenzi wa Simba kuweza kujua
ni wapi mahala pa kupata vitu halisi vya Simba na kwa bei nafuu zaidi”
Duka hili si tu litasaidia katika kuongeza mapato kwa
klabu lakini pia litaziba mianya yote ya wale watu wote wasio itakia mema klabu
yetu na kuamua kutengeneza vitu feki vyenye chapa ya Simba, kwakuwa sasa mtu
ukikutwa na bidhaa feki basi mkono wa sheria utakuwa juu yako. Nipende kuwa
sisistiza wanachama, wapenzi na wadau wote wa Simba na soka la Tanzania kwa
ujumla kuwa kwanza tupende vyetu vya nyumani lakini pia tupende kutumia vitu
halisi na kuachana na utamaduni wa mazoea ya kutojali ni kipi halisi na kipi ni
feki” aliongeza Rais Aveva
Akizungumza kwenye ufunguzi huo Mkurugenzi wa kampuni
ya EAG Group Ltd ambao ni washauri na watekelezaji wa masuala ya biashara na
masko kwa klabu ya Simba Bw. Imani Kajula alisema “nadhani sasa wanasimba
tunaweza kufurahia vya kwetu kwani kwa sasa tunajua ni wapi vinapatikana na ni
wapi ukienda huwezi kukutana na kitu feki chenye chapa ya Simba na hapo si
pengine bali ni Simba Sports Shop lililopo katika jingo la DarFree Market.
Pamoja na kuwepo kwa duka hili lakini pia vifaa vyote vitakavyokuwa
vikipatikana hapa ndani ya siku za hivi karibuni vitakuwa vikipatikana kwenye
duka mtandao (Online Shops) na hivyo kuweza kuwafikia watu wote popote walipo
nchini Tanzania”.
Unapotaka vifaa vyenye ubora wa hali ya juu hakuna
sehemu nyingine zaidi ya Simba Sports Shop. NUNUA HALISI ICHANGIE TIMU YAKO. Alimalizia
Mkurugenzi wa EAG Group Ltd Imani Kajula
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa duka hilo msimamizi
wa Duka la vifaa vya michezo venye chapa ya Simba mkurugenzi
wa kampuni ya Insight Media Bw. Tahir Othman ambao ni waamiliki wa Dukakwa kuhamasisha wapenzi wote wa Soka Tanzania kuweza
kuunga mkono juhudi zinazofanywa na klabu ya Simba ili kuweza kukuza mapato kwa
klabu yetu lakini pia kuweza kupata bidhaa bora na halisi za chapa ya Simba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ SIMBA YAZINDUA DUKA LA VIFAA VYA MICHEZO ”
Post a Comment