Friday, February 5, 2016
SERIKALI YAJIELEZA BUNGENI KINACHOSABABISHA UMEME UKATIKE MARA KWA MARA
Do you like this story?
Serikali
imesema tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara nchini linatokana na
uchakavu na kuzidiwa kwa vituo vya kupoza umeme na miundombinu ya usafirishaji
na usambazaji nishati hiyo.
Katika
kukabiliana na tatizo hilo Tanesco inachukua hatua za kujenga mifumo ya njia
kubwa za umeme wa msongo wa kilovoti 400 (Iringa- Dodoma-Singida-Shinyanga),
gridi ya Kaskazini Mashariki (Dar es Salaam, Chalinze,Tanga –Arusha), ya
Kaskazini Magharibi (Geita- Kagera –Katavi- Kigoma- Rukwa na Mbeya) na
Makambako- Songea wa kilovoti 220.
Kauli hiyo
ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani
wakati akijibu swali la Mbunge wa Magu, Boniventure Kiswaga (CCM).
Kiswaga alitaka
kufahamu serikali imejipangaje kukabiliana na tatizo la kukatika katika kwa
umeme.
Pia mbunge huyo
alitaka kufahamu, Je serikali itakamilisha lini kupeleka umeme katika vijiji
vya jimbo hilo ikizingatiwa mpaka sasa ni asilimia 20 tu ya vijiji ndiyo vina
umeme.
Kalemani
akijibu swali hilo, alisema tatizo la kukatika kwa umeme linatokana na uchakavu
na kuzidiwa kwa miundombinu ya kupoza umeme pamoja na matukio ya kulipuka kwa
transfoma yanayosababishwa na radi hasa kipindi cha mvua pamoja na wizi wa
mafuta ya transfoma unaofanywa na wananchi wasio waaminifu.
Alisema Tanesco
inakamilisha upanuzi wa usambazaji wa umeme katika majiji makubwa ya Arusha,
Dar es Salaam, na Mwanza ambapo kazi hizo zitahusisha ujenzi wa njia mpya za
umeme na kupanua vituo vya kupoza umeme.
“Kukamilika
kwa kituo cha kupoza umeme cha KIA mkoani Kilimanjaro kumeimarisha upatikanaji
wa umeme maeneo ya Mirerani na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro
(KIA),” alisema Kalemani.
Pia vituo vya
kupoza umeme katika jiji la Dar es Salaam vya Gongo la Mboto, Kipawa, Mbagala,
na Kurasini vitaunganishwa kwa njia ya sakiti mzunguko kutoka Ubungo na
Kinyerezi kuanzia Machi mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SERIKALI YAJIELEZA BUNGENI KINACHOSABABISHA UMEME UKATIKE MARA KWA MARA”
Post a Comment