Friday, February 5, 2016
MATAJIRI YANGA WAMJADILI KIIZA
Do you like this story?
Wilbert
Molandi na Khadija Mngwai
KASI ya kufunga mabao ya mshambuliaji wa Simba, Hamis Kiiza inaonekana kuwa tishio kwa timu pinzani katika Ligi Kuu Bara lakini habari mpya ni kuwa baadhi ya mabosi wa zamani wa timu yake ya Yanga, wamekutana juzi usiku na lengo kuu likiwa ni kumjadili mchezaji huyo raia wa Uganda.

Kiiza ambaye alitemwa na Yanga mwaka juzi kwa madai ya kuwa ameshuka kiwango, yupo kileleni katika orodha ya wakali wa mabao akiwa na mabao 14, sawa na Mrundi wa Yanga, Amissi Tambwe.
Akizungumza na Championi Ijumaa, mmoja wa matajiri wa Yanga alisema walikutana wote kwa pamoja kwa ajili ya kujadili mwenendo wa timu yao kwenye mechi zilizobakia ili kuhakikisha wanatetea taji lao la ubingwa wanalolishikilia.
Tajiri
huyo alisema mbali na mwenendo wa timu yao, pia walimjadili Kiiza kutokana na
kasi yake ya ufungaji tangu ametua kuichezea Simba mwanzoni mwa msimu huu.
Alisema walimchambua Mganda huyo na kwenda mbali zaidi kujadiliana juu ya mkataba wake na Simba.
Mkutano huo ulifanyika kwenye moja ya hoteli kubwa jijini Dar es Salaam na wamepanga kuendelea kukutana kwa ajili ya majadiliano zaidi.
“Kiiza hakuondolewa Yanga na viongozi,
aliondolewa na benchi la ufundi ambalo ndilo lililokuwa na dhamana ya kuchagua wachezaji.
Kiiza siyo mchezaji mbaya,” alisema tajiri huyo. Gazeti hili lilipowasiliana na
Kiiza juu ya habari hizo na kumuuliza anazipokea vipi, alisema: “Sina taarifa
zozote na nisingependa kulizungumzia hilo kwa kuwa mimi ni mchezaji wa Simba na
nina mkataba, akili yangu nimeielekeza kuitumikia klabu yangu.”
Kiiza aitangazia vita Yanga
Wakati huohuo, Kiiza amejinadi kuwa nia yao ni kuhakikisha wanashinda kila mechi bila kujali wanacheza wapi, hiyo ikiwa na maana hata Yanga ambao watakutana nao baadaye mwezi huu, maana yake kazi ni moja tu, kupata ushindi.
“Nashukuru kuona tunapata ushindi, nia yetu ni kushinda mechi zote zijazo,” alisema Kiiza.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MATAJIRI YANGA WAMJADILI KIIZA”
Post a Comment