Thursday, February 4, 2016

MAN UNITED YAHUSISHWA NA DILI LA PAUNI MILLION 114 KWA NEYMAR




Mshambuliaji wa Barcelona na timu ya taifa ya Brazil, Neymar anatajwa kuwa huwenda akahamia katika ligi kuu ya Uingereza kwa msimu ujao wa 2016/2017 kutokana na matukio yanayoendelea kumkuta nchini Hispania.

Tetesi hizo zimeelezwa na mtandao wa The Sun wa nchini Uingereza ambao ulimkariri baba yake na Neymar akieleza kuwa kuna klabu ipo tayari kutoa Pauni Milioni 144 ili kupata saini ya mtoto wake na klabu hiyo siyo Real Madrid kutokana na staa huyo kuhusishwa na Madrid kwa siku za karibuni.

Ripoti zinaeleza kuwa tangu Agosti mwaka jana, Manchester United imekuwa ikihusishwa na kuhitaji kumsajili Neymar na inaonekana kuwa mstari wa mbele kumpata mchezaji huyo kama akiwekwa sokoni ikifuatiwa na Chelsea na Manchester City.

Neymar ambaye kwa siku za karibuni alifikishwa mahakamani kwa kuhusishwa na vitendo vya rushwa na udanganyifu na ameisaidia klabu yake ya Barcelona kwa kufunga magoli 21 na kutoa pasi za magoli 13 kwa msimu huu.

0 Responses to “ MAN UNITED YAHUSISHWA NA DILI LA PAUNI MILLION 114 KWA NEYMAR”

Post a Comment

More to Read