Monday, February 1, 2016
SASA MKOA WA DAR KUWA NA WILAYA TANO
Do you like this story?
Rais Dk. John
Magufuli ameidhinisha kuwepo kwa wilaya tano katika jiji la Dar es Salaam,
badala ya tatu zilizokuwepo awali, ili kuleta maendeleo ya haraka hususan
katika elimu.
Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam, Said Sadiki, alisema juzi kuwa, waliwasilisha ombi la ugawaji wa
wilaya za Kinondoni na Temeke kwa rais, ambapo ameshaliidhinisha.
“Hatua
hii ya kuwepo kwa wilaya tano italiwezesha jiji la Dar es Salaam, kupata
maendeleo ya haraka kwa kugawanywa kwa wilaya hizo, ambapo kutakuwa na
usimamizi thabiti na hakutakuwa na kisingizio cha kuelemewa kwa majukumu kwa
watendaji,”alisema.
Aliomba katika
ugawaji wa wilaya hizo, rasilimali zilizopo na mipaka igawanywe kwa manufaa ya
wananchi wa wilaya hizo.
Aidha, alisema
kinachosubiriwa ni ugawaji wa mipaka na kutangazwa rasmi kuongezeka wilaya
mbili ya Kigamboni na Ubungo na kufikisha idadi ya wilaya tano katika jiji la
Dar es Salaam.
Akizungumzia
ombi la ugawaji wa wilaya za Kinondoni na Temeke, Sadiki alisema hadi kufikia
juzi, ombi hilo lilishaidhinishwa na rais, hivyo Kinondoni itakuwa na wilaya
mbili za Kinondoni na Ubungo huku wilaya ya Temeke ikiwa na wilaya za Temeke na
Kigamboni
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ SASA MKOA WA DAR KUWA NA WILAYA TANO”
Post a Comment