Monday, February 1, 2016
MELI KUBWA ILIYOINAMA YAZUA WASIWASI UFARANSA
Do you like this story?
Meli ya kubwa iliyoegemea upande mmoja
inakaribia kufika katika pwani ya Ufaransa, maafisa wa bahari wanasema, ingawa
kuna matumaini ya kuiokoa kabla ya kuzama.
Meli hiyo kwa jina Modern Express ambayo,
imesajiliwa Panama, ilianza kulala upande mmoja Jumanne baada ya kutokea kwa
hitilafu za kimitambo.
Mabaharia wote 22 wameondolewa kutoka kwenye
meli hiyo.
Juhudi za kuisimamisha zimefeli, lakini
maafisa wanasema jaribio jingine litafanywa leo Jumatatu.
Juhudi za leo zikishindikana, basi meli hiyo
itagonga pwani ya Ufaransa kati ya Jumatatu usiku na Jumanne asubuhi.
Hali mbaya ya hewa ilitatiza juhudi za
uokoaji Jumapili.(VICTOR)
Meli hiyo imebeba tani 3,600 za mbao na
mashine kadha za uchimbaji, na imeinama kwa pembe ya kati ya nyuzi 40 na 50.
Ina tani 33 za mafuta.
Mwaka
2002, meli ya kusafirisha mafuta kwa jina Prestige ilizama karibu na pwani ya
Uhispania na kumwaga mafuta tani 50,000 na kuchafua eneo kubwa la bahari.CHANZO:BBC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MELI KUBWA ILIYOINAMA YAZUA WASIWASI UFARANSA”
Post a Comment