Monday, February 1, 2016
MAHAKAMA YASHUSHA RUNGU KWA MAJANGILI...YAWAPIGA KIFUNGO CHA MIAKA 20 AU FAINI YA SH MLIONI 270
Do you like this story?
Mahakama ya
Wilaya ya Manyoni, mkoani Singida, imewahukumu mtu na kaka yake, kutumikia
kifungu cha miaka 20 kila mmoja na kulipa fidia ya sh. milioni 270, baada ya
kuwatia hatiani kwa makosa ya kukutwa na meno ya tembo, silaha na risasi
kinyume cha sheria.
Washitakiwa hao
ni Nicodem Mchongareli na Festol Mchongareli, ambao walikuwa wakikabiliwa na
kesi ya uhujumu uchumi namba 13 ya mwaka jana.
Wanadaiwa
kukutwa na meno ya tembo mawili yenye thamani ya sh. milioni 27, bunduki tatu
zikiwemo za aina ya Riffle, risasi 25 na maganda yake 15.
Hukumu hiyo
ilitolewa na Hakimu Mkazi Joyce Minde, baada ya upande wa Jamhuri uliokuwa
ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Salim Msemo na ule wa utetezi kufunga ushahidi.
Akisoma hukumu
hiyo, Hakimu Joyce alisema wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo, upande wa
jamhuri ulileta mashahidi watano na washitakiwa baada ya kuonekana wana kesi ya
kujibu walijitetea wenyewe.
“Mahakama
imewaona washitakiwa hao wana hatia baada ya upande wa Jamhuri kuthibitisha
mashitaka dhidi yao pasi na kuacha shaka yoyote,” alisema.
Hakimu huyo
aliwapa adhabu washitakiwa hao kwa kukutwa na meno ya tembo, kutumikia kifungo
cha miaka 20 jela kila mmoja na kulipa serikali sh. milioni 270.
Pia shitaka la
pili wamehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya
sh. milioni 333 na makosa mengine kutumilia kifungo cha miaka miwili au kulipa
faini ya sh. milioni mbili kwa kila shitaka.
Adhabu za
vifungo zinakwenda sambamba, hivyo washitakiwa hao watatumikia kifungo cha
miaka 20 kila mmoja
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAHAKAMA YASHUSHA RUNGU KWA MAJANGILI...YAWAPIGA KIFUNGO CHA MIAKA 20 AU FAINI YA SH MLIONI 270 ”
Post a Comment