Tuesday, March 22, 2016

KIKWAZO CHA USAWA WA KIJINSIA KATIKA UONGOZI HIKI HAPA.


Afisa  Programu wa TGNP  mtandao , Scholastica Makwaia akitoa Shukrani kwa Waandishi wa Habari  ambao ameudhuria semina hiyo ya siku mbili jijini Mbeya(Picha na David Nyembe wa Fahari News)

Baadhi ya Waandishi wa Habari kutoka Vyombo Mbalimbali  wakisikiliza kwa makini semina Hiyo.


Baadhi ya Waandishi wa Habari kutoka Nyombo Mbalimbali  wakisikiliza kwa makini semina Hiyo.


Baadhi ya Waandishi wa Habari kutoka Nyombo Mbalimbali  wakisikiliza kwa makini semina Hiyo.(Picha na David Nyembe wa Fahari News)

Samweli Ndoni Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Tanzania Daima akisikiliza kwa makini.(Picha na David Nyembe wa Fahari News)
Baadhi ya Waandishi wa Habari kutoka Nyombo Mbalimbali  wakisikiliza kwa makini semina Hiyo.(Picha na David Nyembe wa Fahari News)

Baadhi ya Waandishi wa Habari kutoka Nyombo Mbalimbali  wakisikiliza kwa makini semina Hiyo(Picha na David Nyembe wa Fahari News).





SAMWEL NDONI, MBEYA
IMEELEZWA kuwa moja ya sababu ya kutofikia malengo ya hamsini kwa hamsini katika nafasi za uongozi kati ya wanaume na wanawake katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana ni wananchi kutopewa fursa ya kushiriki zoezi la kuchagua kuanzia kwenye mchakato wa kura za maoni ndani ya vyama vya siasa pamoja na kutawala kwa vitendo vya rushwa.


Hayo yamebainishwa leo wakati wa kufunga semina ya siku mbili ya mrejesho wa uraghibishi 2016 kutoka Kata ya Igale wilayani Mbeya kati ya mtandao wa jinsia nchini TGNP na waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya.


Wakizungumza katika semina hiyo baadhi ya waandishi wahabari walisema kuwa sababu kubwa iliyopelekea wanawake kutopewa nafasi ya kugombea kuanzia kwenye nafasi ya Ubunge na Udiwani katika uchaguzi mkuu uliopita ni vyama vya siasa kuwachagua wagombea kwa utashi wao badala ya kuwashirikisha wananchi.


Mmoja wa waandishi wa habari washiriki katika Semina hiyo Fredy Jackson (Mbeya fm) alisema kuwa kuna wanawake wenye uwezo wa kufanya kazi kama walivyo wanaume ndani ya jamii hivyo wananyimwa fursa ya kufanya hivyo kutokana na utashi wa wanasiasa kwenye mchakato wa kuwatafuta wagombea.


“Ni vizuri wananchi wawe wanashirikishwa kuchagua viongozi wanaowataka kuanzia ngazi ya mchakato ndani ya vyama hiyo ingesaidia wanawake wengi kupewa ridhaa ya kugombea kwa sababu wanatokea ndani ya jamii zetu” alisema.


Keneth Ngelesi mwandishi wa habari wa Tanzania Daima amesema kutojiamini mila potofu na elimu duni waliyopata wanawake wengi ni sababu inayopelekea wengi wao kutojitokeza kugombea nafasi za uongozi.


Amesema kuwa ni jukumu la jamii kumuandaa na kumkubali kiongozi mwanamke ikiwa ataonesha nia katika nafasi mbalimbali kwani nao wanauwezo sawa na mwanaume ikiwa watapewa fursa.


Joachim Nyambo mwandishi wa habari wa gazeti la Habari leo amesema kuwa kuwepo kwa vitendo vya rushwa ndani ya  mchakato wa kura za maoni ni kikwazo kwa wanawake kupewa nafasi ya kugombea.


“Shida inaonekana ni Rushwa, hivyo unakuwa wale wenye fedha na majina makubwa ndio wanaopata nafasi na wengine wanaachwa, na utaona wanawake wengi hawana sifa hizo.”alisema


Kwa upande wake Afisa  Programu wa TGNP  mtandao , Scholastica Makwaia alisema kuwa kati ya majimbo 264 ya uchaguzi Tanzania bara majimbo 25 pekee ndio yaliyochukuliwa na wanawake.


Katika semina hiyo TGNP, ilikuwa ikitoa mrejesho wa tafiti katika kata ya Igale baada ya kubaini kuwepo kwa changamoto nne katika kata hizo ambazo ni Kilimo,Afya, Maji na Elimu.
MWISHO

0 Responses to “KIKWAZO CHA USAWA WA KIJINSIA KATIKA UONGOZI HIKI HAPA.”

Post a Comment

More to Read