Saturday, April 2, 2016
MBEYA CITY WAICHARAZA COASTAL UNION 4 - 0 KATIKA UWANJA WA SOKOINE MBEYA
Do you like this story?
Mashabiki wa Mbeya City wakishangilia mara Baada ya kupata Goli.(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Wachezaji wa Mbeya City Fc wakishangilia Baada ya kuapata Goli(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Mbeya city
fc yaibuka na ushindi wa magoli manne kwa sifuri dhidi ya Coastal Union kutoka
Tanga katika uwanja wa sokoine mjini Mbeya,ambapo mpira ulianza kwa kasi huku
timu zote mbili zikiwa zinashambuliana.
Goli la kwanza la timu ya Mbeya city fc
lilifungwa mnamo dakika ya 3 ya mchezo kupitia kwa Salvatory Nkulula,ambapo
uzembe wa golikipa wa Coastal union aliweza kuigharimu timu yake baada ya
kuutema mpira uliopigwa kwa adhabu.
Mpira uliendelea kwa kasi yakushambulina
kipindi chote cha kwanza cha mchezo na goli hilo lilidumu kwa kipindi chote cha
kwanza mpaka pale timu ya Mbeya city fc walipopata goli la pili dakika ya 57 ya
mchezo kupitia kwa Salvatory huku akipokea pasi nzuri kutoka kwa Hassani
Mwasapili na kuipatia timu ya Mbeya city fc goli la pili.
Mchezo safi uliooneshwa na timu zote mbili
huku ukiwa unashuhudiwa na mgeni rasmi waziri wa habari,utamaduni,sanaa na
michezo Mh Nape Moses Nnauye pamoja na mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh Amos Gabriel
Makalla Goli la tatu lilipatikana mnamo dakika ya 74 likifungwa na Hassan
Mwasapili ambapo aliweza kuwainua mashabiki wa timu ya Mbeya city fc baada ya
kupiga kwa ufundi mkubwa na mpira kuingia moja kwa moja katika nyavu za timu ya
Coastal union,huku goli la nne likiwekwa nyavuni dakika ya 87 kupitia kwa
Ditram Nchimbi na kukamilisha jumla idadi ya magoli manne.
Huku waziri wa habari,utamaduni,sanaa na
michezo Mh Nape Moses Nnauye akisisitiza katika michezo si sehemu ya kuleta
mambo ya vyama kwani yatafanya Timu za Mbeya kushuka pamoja na mambo mengine ambayo yanaweza
kudidimiza michezo katika nchi ya Tanzania.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MBEYA CITY WAICHARAZA COASTAL UNION 4 - 0 KATIKA UWANJA WA SOKOINE MBEYA ”
Post a Comment