Tuesday, April 5, 2016
PAMOJA NA KURIDHISHWA NA UKARABATI WA SHULE, MKUU WA MKOA WA MBEYA ATOA AGIZO JIPYA KUHUSU IYUNGA SEKONDARI.
Do you like this story?
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Amosi Makalla akihoji jambo kabla ya kuanz akukagua(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Amosi Makalla akisalimiana na Meya wa Jiji la Mbeya Mh David Mwashilindi mara Baada ya kuawasili Shuleni Hapo Iyunga.(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Amosi Makalla akikagua Miundombinu ya maji katika vyoo vya mabweni katika Shule ya Sekondari Iyunga.(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Mkuu wa
mkoa wa Mbeya Amos Makala amempongeza mkuu wa Wilaya ya Mbeya, ndg Nyirembe
Munasa na kumshukuru kwa kazi kubwa ya kuirejesha shule ya Sekondari ya Iyunga
katika hali yake ya awali na kuiboresha vema baada ya majanga mawili mawili ya
moto yaliyotokea mfululizo katika mwezi Machi mwaka huu.
Mkuu wa
mkoa wa Mbeya pia ameishukuru wizara ya TAMISEMI chini ya afisi ya rais kwa
kuuvaa uhusika wa kuilea shule ya sekondari Iyunga baada ya kupata matatizo ya
moto kwani shule zote za sekondari na msingi nchini Tanzania ziko chini ya
wizara ya TAMISEMI.
Akitolea
mifano ya methali mbili ambazo ni "ukondefu wa mbwa ni udhaifu wa mwenye
mbwa" na "Mafanikio yana marafiki wengi, matatizo mtoto yatima"
mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makala amewashukuru watanzania waliotoa michango
mbalimbali na kuungana pamoja katija kipindi hiki kigumu cha matatizo ili
wanafunzi warejee shuleni aprili mosi.
Mkuu wa
mkoa pia ameonesha kufurahia kile kinachoonekana sasa katika shule ya Iyunga
kwani baada ya majanga ya moto kutokea na kutolewa agizo la kukarabati majengo
yaliyoathiriwa na moto, hata yale majengo ambayo hayakuwa katika mpango wa
kukarabatiwa nayo pia yanakarabatiwa.
Pamoja na hayo Makala ametoa agizo la kuwekwa
hadharani kwa taarifa ya fedha kwa kutanabaisha kila kilichofanyika katika
harambee ikiwa ni pamoja na kuthaminisha hesabu zote zilizofanyika na kuwekwa
katika makaratasi ya taarifa. Pamoja na agizo hilo, mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos
Makala ametoa agizo la kukarabatiwa mabweni yote ya shule ya Sekondari ya
Iyunga na baada ya hapo itafuata kazi ya kukarabatiwa kwa nyumba za waalimu.
Wakati
akitoa maagizo hayo Makala amewataka madiwani wote wa halmashauri ya jiji la
Mbeya kufanya kazi pamoja naye pasipo kujali itikadi za vyama na kuahidi kuwa
atakuwa tayari kushirikiana na kila diwani ili mambo yaende sawa huku akitumia
kauli ya 'HAPA KAZI TU' Shule ya sekondari Iyunga ya hapa jijini Mbeya ilipatwa
na majanga mawili ya moto mfululizo kufuatia uchakavu wa miundombinu ya umeme
katika majengo ya shule hiyo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “PAMOJA NA KURIDHISHWA NA UKARABATI WA SHULE, MKUU WA MKOA WA MBEYA ATOA AGIZO JIPYA KUHUSU IYUNGA SEKONDARI.”
Post a Comment