Thursday, April 21, 2016
NMB YAZINDUA BUSINESS CLUB IFAKARA.
Do you like this story?
NMB
imeendelea kuwa kinara katika kubuni na kuboresha huduma mbali mbali za
kibenki, ili kuwawezesha wateja wake kupata unafuu na urahisi wa upatikanaji wa
huduma za kibenki nchini Tanzania. NMB pia inatambua mahitaji ya wateja
yanatofautiana, hivyo basi uzinduzi wa NMB Business Clubs una lengo la
kuwafikia wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa walioko Ifakara na Wilaya
ya Kilombero kwa Ujumla. Wafanyabiashara hawa ni sehemu ya wafanyabiashara
zaidi ya 50,000 ambao ni wateja wa NMB nchi nzima.
Hii
ni Business Club ya 33 kuzinduliwa na NMB ambapo nyingine ziko katika mikoa
tofauti nchi nzima, na kuna mpango wa kuongeza moja zaidi kabla ya mwisho wa
maka. Dhumuni kubwa ni kuwaunganisha wafanyabiashara wote nchini waweze
kufaidika na huduma za NMB ambazo pia zitawawezeshakujikimu kimaisha. Hadi sasa
NMB Business Clubs zina zaidi ya wafanyabiashara 10,000 waliojiunga.
Bottom of Form
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ NMB YAZINDUA BUSINESS CLUB IFAKARA.”
Post a Comment