Thursday, April 21, 2016
WATU WANNE WATIWA MBARONI SENGEREMA KWA KUNYWA POMBE MCHANA
Do you like this story?
Wilaya ya
Sengerema imeanza kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais baada ya kukamata watu
wanane waliokutwa wakinywa pombe saa za kazi.
Amri ya kukamatwa
na kuwekwa mahabusu kwa watu hao ilitolewa juzi na Mkuu wa Wilaya Zainabu
Terack baada ya kukuta baa zimefunguliwa asubuhi zikiwa na wateja waliokuwa
wakipata kinywaji kabla ya saa 9:30 alasiri, muda ambao ofisi za Serikali
hufungwa.
Rais John
Magufuli alitoa agizo hilo la kupiga marufuku unywaji pombe na uchezaji pool
nyakati za kazi wakati alipokuwa akiwaapisha wakuu wa mikoa mwezi uliopita.
Alitaka vijana ambao watakaidi maelezo ya kuambiwa, nguvu itumike kuwalazimisha
kufanya kazi.
Kwa mujibu
wa mkuu huyo wa wilaya, aliyeongoza oparesheni ya dakika 45 ya kusaka
wanaokunywa pombe na kucheza pool muda wa kazi, watuhumiwa hao watafikishwa
mahakamani kwa makosa ya uzembe na kukiuka amri halali ya serikali.
Wakijitetea
baada ya kutiwa mbaroni, baadhi ya waliokamatwa walidai kuwa walienda baa
kujiliwaza wakati wa msiba wa ndugu yao waliyemtaja kwa jina la Petro Shoyo, na
kumwomba mkuu wa wilaya kuwasamehe kwa sababu ni kosa lao la kwanza.
Lakini
mkuu huyo wa wilaya alisisitiza wapelekwe mahakamani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WATU WANNE WATIWA MBARONI SENGEREMA KWA KUNYWA POMBE MCHANA”
Post a Comment