Monday, April 18, 2016
MVUA YASABABISHA MADHARA KAYA 156 ZAKOSA MAHALI PAKUISHI, NYUMBA 70 MBEYA.
Do you like this story?
Mtoto akiwa amebeba vyombo mara baada ya Mvua kupungua..(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Familia ikiwa inatoa Mahindi yaliyokuwa ndani ya nyumba na kuyasafisha mara baada ya Mvua Kukatika.(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Mahindi yakiwa yamejaa matope..(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Ikawabidi kubuni Njia Mbadala .(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
KAYA 156
katika kata ya Igawilo jijini Mbeya hazina mahali pa kuishi kutokana na nyumba
zao kuzingirwa na maji kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini hapa.
Mbali na
kukosa mahali pa kuishi kaya hizo pia zimepoteza mali zao kadhaa yakiwemo
mavazi, samani za ndani, mifugo pamoja na vyakula.
Athari
hizo zimetokana na mvua zilizoanza kunyesha Aprili 15 jioni na kusababisha
maeneo mengi ya Jiji la Mbeya kujaa maji na kuharibu miundombinu kadhaa
yakiwemo madaraja katika kata ya Nzovwe, Ituha na Iyunga
Katika
kadhia hiyo nyumba 70 zimejaa maji na tope na kusababisha wakazi wake kukosa
mahali pa kuishi.
Akizungumza Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwanyanje, Eliya Philemon, alisema athari
hizo zimetokana na maji yanayotiririka kutoka maeneo ya milimani kujaa kwenye
nyumba hizo kutokana na wakazi wake kujenga kwenye mikondo ya maji.
Alisema,
mbali na wananchi hao kujenga kando ya mikondo ya maji pia mmiliki wa kituo cha
Mafuta cha Lake Oil kilichopo katika eneo hilo ameziba mitaro inayopitisha maji
kwenda kwenye mikondo ya maji hali inayochangia nyumba hizo kuzingirwa na maji.
Kutokana
na hali hiyo,Mstahiki Meya wa jiji la Mbeya, David Mwashilindi, ameuagiza
uongozi wa jiji kuhakikisha mmiliki wa kituo hicho anazibua mfereji huo ili
kuondoa changamoto hiyo inayosababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi wa eneo.
Baaadhi ya
wakazi wa eneo hilo wameulaumu ouongozi wa jiji la Mbeya kwa madai ya kushindwa
kusimamia ujenzi wa makazi kwa kufuata utaratibu wa mipango miji hali
iliyosababisha wananchi kujenga bila kufuata taratibu husika na hatimaye
kutokea kwa kadhia hiyo.
Kwa upande
wake Kaimu Mkurugenzi wa jiji la Mbeya, Samuel Lazaro, alisema hadi sasa bado
wanaendelea kufanya tathmini kuhusu ukubwa wa kadhia hiyo ili kupata takwimu
sahihi zauharibifu wa mali na athari zilizowapata wananchi hao ili kujua
jukubwa na aina ya misaada wanayopaswa kuitoa kwa waathirika hao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MVUA YASABABISHA MADHARA KAYA 156 ZAKOSA MAHALI PAKUISHI, NYUMBA 70 MBEYA.”
Post a Comment