Thursday, April 14, 2016
OMBAOMBA WAANZA KUONDOLEWA JIJINI DAR.
Do you like this story?
Agizo la Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda limeanza kufanyiwa kazi baada ya
karandinga kuanza kuwasomba ombaomba waliojaa katika maeneo mengi jijini hapa.
Makonda
alitangaza kuanza kuwaondoa ombaomba hao juzi, huku akipiga marufuku wananchi
kuwapa pesa kwa kuwa ndicho chanzo cha kuwapo kwao jijini hapa.
Zoezi hilo la
kuwaondoa watu hao lilianza juzi usiku katika maeneo ya Mnazi Mmoja, Samora na
Kariakoo.
Jana maeneo
mbalimbali ambayo aghalabu ombaomba hupenda kukaa yalikuwa tupu.
Maeneo hayo
ikiwamo barabara ya Morocco, Magomeni Usalama, Fire na Baridi hayakuwa na watu
wa kundi hilo.
Mmoja wa
ombaomba aliyekuwa na watoto wawili alipomuona mwandishi wa habari hizi katika
maeneo ya Fire, alitimua mbio na kujificha pembeni mwa barabara, huku akisema: “Tumetoka
Dodoma, hatutaki kurudi.”
Kadhalika,
operesheni hiyo licha ya timuatimua kuwakumba ombaomba, wapigadebe nao
wameunganishwa katika kundi hilo kwa kuanza kuondolewa kwenye vituo vya mabasi.
Baadhi ya
wapigadebe hao wamedai ni vigumu kwa Makonda kuwaondoa kwa kuwa wanachofanya ni
kwa manufaa ya maisha yao na hawana pa kwenda.
Agizo la kutaka
ombaomba wakamatwe na kuondokana na vitendo hivyo liliwahi kutolewa pia na
waliowahi kuwa wakuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Yusuf Makamba, Abbas Kandoro na
Said Mecky Sadiki.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ OMBAOMBA WAANZA KUONDOLEWA JIJINI DAR.”
Post a Comment