Saturday, April 30, 2016
TAARIFA KAMILI KUHUSU AJALI YA BASI LA HBS LILILOKUWA LINATOKA MBEYA KUELEKEA TABORA,LAUA WATU WA NNE NA KUJERUHI 29.MBEYA
Do you like this story?
Mwonekano wa Basi la Hbs Express mara Baada ya kupata Ajali katika Eneo la Maji Mazuri katika Barabara ya kutoka Mbeya kwenda Chunya.(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Wasamalia wema wakiokoa watu waliokuwa wamenasa ndani ya Basi hilo(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Polisi wa Usalama Barabarani akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla mara Baada ya kufika katika eneo la Ajali (Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
wananchi wakiwa wamembeba Mmoja wa walionusurika katika Ajali Hiyo(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Baadhi ya vijana wakiwa wanachimba shimo ili kuweza kutoa mwili wa mmoja wa Abilia aliyekuwa ameminywa na Basi hilo.(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla akimpa pole mama na Mwanae walionusurika katika Ajali Hiyo katika Hospitali ya Rufaa(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
WATU
wanne wamepoteza maisha na 29 kujeruhiwa katika ajali ya basi la abiria aina ya
scania lenye namba za usajili T273 AHV mali ya kampuni ya HBS baada ya kuacha
njia na kupinduka kandokando ya barabara katika eneo la Maji mazuri lililopo
Wilayani Mbeya.
Basi
hilo likiendeshwa na dereva Nassoro Hemedy, linalofanya safari zake za mikoani
lilikuwa likitokea Mkoani Mbeya na kuelekea Mkoani Tabora, lilipata ajali hiyo
majira ya saa mbili za asubuhi, baada ya kudaiwa kufeli breki na kisha
kupinduka.
Katika
ajali hiyo, watu wanne ambao wanawake wawili na wanaume wawili walipoteza
maisha huku 29 wakijeruhiwa lakini kwa mujibu wa taarifa ya muuguzi wa zamu wa
hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Jesca Kahangwa majeruhi 20 hali zao si nzuri na
wanaendelea kupatiwa matibabu.
Aidha,
katika hali isiyokuwa ya kawaida, mtoto wa miaka 15 Yakob Mahonga ambaye ni
mmoja wa abiria aliyenusurika katika ajali hiyo, aliweza kuwaokoa baadhi ya
abairia kwa kuwafungua mikanda, kisha kuvunja vioo vya basi ili waweze
kujiokoa.
Akizungumza
mtoto huyo ambaye ni mzaliwa wa Mkoa wa Arusha, amesema kuwa alikuwa akisafiri
na mjomba wake kuelekea Wilayani Chunya kwa ajili ya kwenda kumuona mgonjwa.
“Tulipofika
katika eneo la Kawetele mbali kidogo na eneo la ajali mimi nikiwa nimekaa pembeni
ya dereva nilianza kuhisi kwamba gari hilo linatatizo baada ya kumuona dereva
akiwa anahangaika,”alisema.
Alisema,
walipofika kituo kingine cha mbele gari hiyo ilisimama na kasha kondakta wa
gari na dereva walishuka na kuanza kurekebisha baadhi ya vitu vilivyokuwa
haviko sawa chini ya gari, lakini walihangaika kutafuta maji na kuyakosa na
safari kuendelea.
“Dereva
na kondakta walinijibu kuwa hawafahamu zilipo na kubaki ni kimshuhudia dereva
akiruka kutokea dirishani, lakini nilihangaika kutafuta spana hizo na
kufanikiwa kuzipata na kuanza kuwafungua abiria mikanda na kisha kuvunja vioo
vya basi ili waweze kutoka nje,”alisema.
Akizungumzia
ajali hiyo kwenye eneo la tukio, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amosi Makala, ambaye
mbali na kutoa pole kwa majeruhi lakini alitumia nafasi hiyo kuliagiza jeshi la
polisi Mkoani Mbeya, kitengo cha usalama barabarani kuhakikisha wanafanya
ukaguzi wa magari katika kituo cha mabasi kabla ya kuanza safari zake.
Hata
hivyo, Mkuu huyo ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya
Mkoa wa Mbeya,alikitaka kitengo cha uslama wa barabarani kutoa taarifa ni kwanini
gari hilo liliruhusiwa kusafiri huku likiwa limebeba abiria zaidi ya 80.
“Nimeambiwa
gari hili lilikuwa limebeba abiria waliokuwa wamesimama si chini ya 20 kutoka
stendi ya mabasi, hivyo ninawataka wahusika kunipa maelezo ya kutosha na kwa
hili, sintalifumbia macho wahusika wa uzembe huu watawajibika hatuwezi kuweka
maisha ya watu rehani,”alisema.
Mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TAARIFA KAMILI KUHUSU AJALI YA BASI LA HBS LILILOKUWA LINATOKA MBEYA KUELEKEA TABORA,LAUA WATU WA NNE NA KUJERUHI 29.MBEYA”
Post a Comment