Wednesday, June 8, 2016

AMOSI MAKALLA: BARABARA ZOTE ZILIZO CHINI YA KIWANGO ZIRUDIWE MARA MOJA. MBEYA


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Amosi Makalla Akikagua Barabara mara Baada ya kufanya Ziara katika maeneo Mbalimbali ya Jiji la Mbeya Pia akiambatana na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji Mussa Mapunda(mwenye shati la Blue) na Mhandisi Oswald Kasamballa(kulia)




Mkandarasi akiwa katika eneo la kazi Kuziba Sehemu ambazo Zimeharibika.



Mwananchi akitoa kero zake kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Amosi Makalla mara Baada ya kufanya Ziara ya kukagua Barabara zilizojengwa na Mradi wa Bank ya Dunia.(Picha na David Nyembe wa Fahari News)


Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala ameuagiza uongozi wa jiji la Mbeya kuhakikisha wanasimamia ukarabati wa barabara zote za jiji zinazodaiwa kujengwa chini ya kiwango.
Makalla amesema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua barabara kadhaa jijini hapa zilizojengwa na serikali kupitia mradi ya banki ya dunia.

Amesema barabara hizo zinatakiwa kurudiwa kwa kiwango cha ubora kwa kile alichoeleza kuwa barabara hizo zimegharimu kiasi cha fedha zaidi y ash.bilioni 23 ambapo amewataka pia madiwani wa halimashauri ya jiji kuhakikisha wanasimamia fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

Hata hivyo mhandisi wa barabara jiji la mbeya Oswald Kasambala amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kuahidi kukarabati barabara hizo upya na kwamba miongoni mwa sababu za kuharibika barabara hizo ni magari yenye uzito mkubwa kutumia barabara hizo ambazo tayari zimeanza kufanyiwa maboresho ikiwa ni pamoja na upanuzi wa mitaro ya maji
Baadhi ya wananchi waliopata fursa ya kutoa malalamiko yao kwa mkuu wa mkoa wamedai kuwepo kwa kero ya maji kujaa hususani nyakati za mvua hivyo kuiomba serikali kuhakikisha barabara zinazojengwa zinakidhi matakwa ya jamii.

0 Responses to “AMOSI MAKALLA: BARABARA ZOTE ZILIZO CHINI YA KIWANGO ZIRUDIWE MARA MOJA. MBEYA”

Post a Comment

More to Read