Saturday, June 11, 2016

VIDEO: UFARANSA YAANZA VYEMA MASHINDANO YA EURO 2016





Wenyeji wa mashindano ya EURO 2016, Ufaransa wamefungua mashindano hayo kwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi  ya Romania, mchezo ulioshuhudiwa na mashabiki 75,113 katika dimba la Stade de France lililopo katika jiji la Paris.

Ushindi wa Ufaransa ulipatikana kupitia mshambuliaji Olivier Giroud katika dakika ya 57 baada ya kuunganisha kwa kichwa mpira mrefu uliopigwa na Dimitri Payet na Payet mwenyewe kufunga goli la pili na la ushindi katika dakika ya 89 baada ya kupiga shuti kali lililomshinda goli kipa wa Romania, Ciprian Tatarusanu.

Goli pekee la Romania katika mchezo huo lilifungwa na Bogdan Stancu kwa njia ya penati baada ya beki wa Ufaransa, Patrice Evra kumchezea faulo mchezaji wa Romania, Stanciu.

Kwa matokeo hayo, Ufaransa imekuwa kinara wa kundi A ikiwa na alama tatu na Romania ikishika mkia wa kundi hilo.
Michezo inayotaraji kuchezwa leo Jumamosi ni, Albania na Switzerland majira ya saa 16:00 jioni, Wales na Slovakia saa 19:00 usiku na England na Urusi saa 22:00 usiku.

0 Responses to “ VIDEO: UFARANSA YAANZA VYEMA MASHINDANO YA EURO 2016”

Post a Comment

More to Read