Saturday, June 11, 2016
TAREHE YA MWISHO YA KULIPA KODI YA MAPATO NA KODI YA ONGEZEKO LA THAMANI (VAT)
Do you like this story?
Walipakodi wote wanakumbushwa
kuzingatia mwisho wa kulipa kodi ya Mapato na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)
PASIPO ADHABU
1.O ULIPAJI WA
KODI YA MAPATO – MAKADIRIO YA AWALI
⦁ walipakodi wote ambao hesabu zao za
mizania zinaishia tarehe 30/06/2016, wanapaswa kulipa sehemu ya nne ya
makadirio ya awali ya mwaka 2016
⦁ walipakodi wote ambao hesabu zao za
mizania zinaishia tarehe 30/09/2016, wanapaswa kulipa sehemu ya tatu ya
makadirio ya awali ya mwaka 2016
⦁ walipakodi wote ambao hesabu zao za
mizania zinaishia tarehe 30/12/2016, wanapaswa kulipa sehemu ya pili
⦁ walipakodi wote ambao hesabu zao za
mizania zinaishia tarehe 31/03/2017, wanapaswa kulipa sehemu ya kwanza ya
makadirio ya awali ya mwaka 2017
Tarehe za malipo kwa ufupi:
Tarehe ya mwisho wa mwaka wa
Mahesabu Awamu za Malipo Tarehe ya Mwisho
wa Malipo bila Adhabu
30/06/2016 Awamu
ya nne ya mwaka wa Mapato 2016 30/06/2016
30/09/2016 Awamu
ya tatu ya mwaka wa Mapato 2016 30/06/2016
31/12/2016 Awamu
ya piliya mwaka wa Mapato 2016 30/06/2016
31/03/2017 Awamu
ya kwanza ya mwaka wa Mapato 2017 30/06/2016
2.0 UWASILISHAJI
WA RITANI ZA MAPATO KWA MWAKA 2016
Walipakodi wote ambao mwaka wao wa
mapato uliisha tarehe 31/12/2015, wanatakiwa kuwasilisha ritani zao pamoja na
hesabu zilizokaguliwa na kulipa kodi yote inayotakiwa mnamo au kabla ya tarehe
30/06/2016
3.0 UWASILISHAJI
WA RITANI ZA VAT ZA MWEZI MEI 2016
Walipakodi wote ambao wamesajiliwa
na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) wanatakiwa kuwasilisha ritani za mwezi mei
2016 na kulipa kodi inayotakiwa kabla ya tarehe 30/06/2016. Pia wale wote ambao
hawakufanya biashara wanatakiwa kuwasilisha ritani zao zisizokuwa na malipo
(NIL RETURN)
4.0 UTOAJI WA
RISITI ZA KODI ZA KIELEKITRONIKI/ ANKARA YA KODI
Walipakodi wote waliosajiliwa na
wasiosajiliwa kwenye kodi ya Ongezeko la Thamani wanakumbushwa Kutoa risiti za
kodi za kielekitroniki/Ankara ya kodi kwa mauzo yote wanayofanya kulingana na
fedha zilizopokelewa. Ni kinyume cha sheria kupokea malipo kwa kuuza Bidhaa au
huduma bila Kutoa risiti ya kodi ya kielekitroniki/Ankara ya kodi
5.0 KUMBUKA
Riba na Adhabu itatozwa/itatolewa
kwa Pointi ya Sarafu (Currency Points) kwa mlipakodi yeyote ambaye hatalipa
kodi kwa muda unaotakiwa au atakayeshindwa kuwasilisha ritani kwa muda
unaotakiwa kwa mujibu wa sheria.
Ili kuepuka msongamano na
usumbufu mwingine walipakodi wanashauriwa kutosubiri siku ya Mwisho.
Tunashukuru kwa ushirikiano mzuri.
“Pamoja
Tunajenga taifa letu”
Imetolewa
na:
Idara
ya Huduma na Elimu kwa mlipakodi
TRA
Makao Makuu
S.L.P
11491
Dar
es Salaam.
Barua pepe: huduma@tra.go.tz
Kituo cha
Huduma
Simu bila
Malipo
0800
780078
0800
750075
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TAREHE YA MWISHO YA KULIPA KODI YA MAPATO NA KODI YA ONGEZEKO LA THAMANI (VAT)”
Post a Comment