Friday, August 19, 2016
MKUU WA MKOA WA MBEYA AFANYA MKUTANO WA HADHARA KYELA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI.
Do you like this story?
| Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla akiongea na wananchi wa Wilaya ya Kyela kusikiliza Kero.(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
| Mmmoja wa wananchi akitoa Kero yake kwa Mkuu wa Mkoa. |
| Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla akiongea na wananchi wa Wilaya ya Kyela kusikiliza Kero.(Picha na David Nyembe wa Fahari News). |
| Mmmoja wa wananchi akitoa Kero yake kwa Mkuu wa Mkoa. |
| Wananchi wakisikiliza kwa makini Majibu ya Kero zao kwa Mkuu wa Mkoa |
MKUU
wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla Leo amefanya mkutano wa hadhara wa kusikiliza Kero
za wananchi mjini Kyela na kuamuru wakuu wa idara ya ardhi, Afya na taasisi
mbalimbali ikiwemo Tanesco na Rea kujibu Kero za wananchi.
Ameitaka idara ya ardhi kuondoa urasimu wa kutoa hati kwa wananchi na amewaagiza Tanesco kufanya kikao na madiwani na wenyeviti wa Vijiji na kuwapa orodha vitakavyopatiwa Umeme awamu ya pili na Tatu.
Amewataka watendaji kubadilika na kuwahudumia wananchi katika kiwango cha juu ili wananchi waone ofisi za serikali ni rafiki kwa wananchi katika kushughulikia kero.
Kuhusu ushuru kwa Mazao na hasa mpunga amewatadharisha rasmi wananchi wa kyela kuwa halmashauri imefuta ushuru kuunga Mkono agizo la mhe Rais kuwaondolea Kero ya ushuru wakulima na ushuru utatozwa kwa wafanyabiashara wanaosafirisha nje ya Wilaya.
Amewahakikishia wananchi kuwa ujenzi wa Barabara unafanyika sasa mjini Kyela z utakuwa wa kiwango cha juu na ujenzi awamu ya kwanza utakamilika tarehe 7 septemba mwaka huu.
Amewataka wananchi kufanya kazi kwa bidii na kujitetea maendeleo na serikali inawahakikishia ushirikiano wa kutosha
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)

0 Responses to “MKUU WA MKOA WA MBEYA AFANYA MKUTANO WA HADHARA KYELA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI.”
Post a Comment