Saturday, August 20, 2016
TANZANIA KUACHANA NA NGUO ZA MITUMBA IFIKAPO MWAKA 2018
Do you like this story?
Na
Beatrice Lyimo-MAELEZO
Serikali
imeazimia kuachana na biashara ya kuingiza nguo za mitumba kutoka nje ya nchi
ifikapo mwaka 2018.
Maazimio
hayo yamebainishwa na Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama katika uzinduzi wa mafunzo
ya uanagenzi ya ushonaji nguo katika kiwanda cha Tanzania Tooku Garments
Company, Ltd.
Mhe.
Jenista Mhagama amesema kuwa katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
wamekubaliana kwamba ifikapo mwaka 2018 soko la Afrika Mashariki halitaingiza
nguo za mitumba kutoka nje.
Ameongeza
kuwa kwa kutekeleza azimio hilo Serikali imeandaa mafunzo ya kuhakikisha
vijana wengi wanapata stadi za kushona nguo nchini ili kuwawezesha kufanya kazi
katika viwanda vilivyopo na vitakavyojengwa kwa ajili ya kutengeneza bidhaa
zetu wenyewe na kuacha kutegemea bidhaa kutoka nje.
“Tumejipanga
kutekeleza azimio hili na kwa kushirikiana na kiwanda hiki tunategemea kutoa
mafunzo ya uanagenzi kwa vijana 2,000 kwa mwaka katika stadi za kubuni mitindo,
kukata, kushona na kumalizia nguo”
alisema Mhe. Jenista.
Aidha
Waziri huyo amewapongeza washiriki wa mafunzo hayo kwani mafunzo hayo
yatawasaidia kuendana na viwango vya soko la kimataifa na mahitaji ya soko la
nguo kwa kutumia teknolojia ya kisasa katika kubuni mitindo, kukata na kushona
nguo zenye ubora wa kimataifa.
“Imani
yangu kuwa wataalamu waliopo katika kiwanda hiki watawapa ujuzi wa kutosha na
wengine wataweza kupata ajira katika kiwanda hiki tumieni fursa hii mliyoipata
ni ya pekee kwani mmebahatika kuwa miongoni mwa wanafunzi wa kwanza kupata
mafunzo chini ya Programu ya Kukuza Ujuzi Nchini.
Mhe
Jenista amesisitiza kuwa mafunzo hayo yatawezesha vijana kupata ajira katika
Viwanda, kujiajiri na hata kutoa ajira kwa wengine hivyo vijana watumie fursa
hiyo kutengeneza mtaji na kujiunga katika vikundi vitakavyowawezesha
kufungua viwanda vidogo vidogo vya kutengeneza nguo na kuendelea kukuza ujuzi
waliopata.
Pia
Waziri Jenista ametoa wito kwa viwanda vingine kushirikiana na Serikali kukuza
ujuzi kwa vijana kupitia mafunzo ya uanagenzi na kuwahakikisha kuwa Serikali
itaendelea kuwawezesha Vijana kupata mafunzo ya aina hiyo.
“Napenda
niwahakikishie kuwa Serikali iko bega kwa bega nanyi, fungueni viwanda vingi
sehemu mbalimbali katika nchi yetu, sisi kama Serikali tutashirikiana kwa
pamoja kuhakikisha rasilimali watu ya kuendesha viwanda hivi inapatikana”
Mbali
na hayo Serikali inayo mipango na mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa
Tanzania inakuwa nchi ya viwanda na kuwa na uchumi wa kipato cha kati ifikapo
mwaka 2025.
Serikali
iliingia makubaliano na kiwanda cha Tanzania Tooku Garments Co. Ltd kutoa
mafunzo ya uanagenzi kwa vijana 2,000 kwa mwaka katika stadi za kubuni mitindo,
kukata, kushona na kumalizia nguo .Jumla ya vijana 1,089 waliomba nafasi ya
kupata mafunzo hayo yatakayoendeshwa kwa awamu tatu na kwa sasa jumla ya vijana
430 wanapata mafunzo hayo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)


0 Responses to “ TANZANIA KUACHANA NA NGUO ZA MITUMBA IFIKAPO MWAKA 2018”
Post a Comment