Saturday, August 20, 2016
SIMBA YAANZA VIZURI LIGI KUU, YAICHAPA 3-1 NDANDA.
Do you like this story?
Simba Ikicheza
mchezo wake wa kwanza kwenye ligi kuu Tanzania bara,Kikosi cha Simba leo
kimeuanza vema msimu huu 2016/17 baada ya kamaliza mchezo wake na Ndanda Fc Kwa
mabao 3 - 1.
Mchezo
uliokuwa mkali na wakuvutia ambapo pande zote mbili zilionekana zenye hamu ya
kuibuka na ushindi wa mchezo wa leo. Kipindi cha kwanza kilimalizika Kwa timu
zote mbili kufungana 1 - 1 ambapo goli la Simba likifungwa na mshambuliji wake
wa kimataifa Laudit Mavugo wakati Ndanda goli lao liliwekwa kimyani na Omary Mponda.
Katika
Kipindi cha pili Simba kuifanya mabadiliko ambayo yaliweza kuisaidia kuongeza
goli la pili likifungwa na mchezaji wake wa kimataifa Blagnon ambaye aliingia akabadilishana
na Ibrahim Ajib. Ndani ya dakika za lala salama Simba ilipata goli la 3 kupitia
mchezaji wake Kichuya ambapo mpaka kipenga cha mwisho kinapigwa Simba 3 - 1
Ndanda Fc
![]() |
| (Picha zote na Robert wa Fahari News) |
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)










0 Responses to “SIMBA YAANZA VIZURI LIGI KUU, YAICHAPA 3-1 NDANDA.”
Post a Comment