Thursday, October 27, 2016
ALIYEKUWA USALAMA WA TAIFA AHUKUMIWA MIAKA MIWILI JELA.
Do you like this story?
Mahakama
ya Wilaya ya Ilala imemhukumu Seleman Manoti, kifungo cha miaka miwili jela kwa
kupatikana na hatia ya kujifanya usalama wa Taifa.
Hata
hivyo, mahakama imetoa hukumu hiyo bila mshitakiwa kuwepo mahakamani kutokana
na kuruka dhamana kesi hiyo ilipokuwa inasikilizwa.
Akitoa
hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi, Flora Haule alisema kuwa upande wa mashitaka,
ulileta mashahidi wanne kwa ajili ya kuthibitisha tuhuma hizo.
Alisema
kutokana na ushahidi uliotolewa, mahakama imeridhishwa na ushahidi huo na
kwamba mahakama inamtia hatiani mshitakiwa licha ya yeye kutokuwepo.
“Hati
ya kumkamata mshitakiwa itolewe na adhabu hii itaanza kutumika pindi mshitakiwa
atakapokamatwa kwani alitoroka akiwa na haki ya kusikilizwa,” alisema Hakimu Haule.
Wakili
wa Serikali, Ester Kyara aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa iwe
fundisho kwa wengine.
Inadaiwa
kuwa Novemba 19, 2014 maeneo ya Kariakoo Msimbazi wilayani Ilala, mshitakiwa
alijitambulisha kwa Issaya Odelo na Charles Odinga kuwa Ofisa Usalama wa Taifa,
kitu ambacho alijua si kweli.
Katika
hatua nyingine, kondakta Ally Salum (23), mkazi wa Mwananyamala, amehukumiwa
kifungo cha miaka mitano jela baada ya kupatikana na hatia ya kuiba daladala.
Mbali
na mshitakiwa huyo, Exavery Kaunga (44) ambaye ni mlinzi na mkazi wa Kiwalani,
Minazi Mirefu, aliachiwa baada ya ushahidi dhidi yake kuwa na shaka.
Akitoa
hukumu hiyo jana katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Hakimu Mkazi Mwandamizi,
Juma Hassan, alisema kuwa upande wa mashitaka ulileta mashahidi wanne
kuthibitisha kosa hilo.
“Nimeridhika
na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka, nakutia hatiani mshitakiwa kama
ulivyoshitakiwa kwa kutumikia kifungo cha miaka mitano jela,” alisema Hakimu Hassan.
Kabla
ya kutolewa adhabu hiyo, Wakili wa Serikali, Grace Mwanga aliiomba mahakama
kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwa wengine. Hata hivyo,
mshitakiwa alipoulizwa ni kwa nini asipewe adhabu kali, hakujibu chochote na
mahakama kutoa adhabu hiyo.
Washitakiwa
hao walishitakiwa kwa makosa mawili ya kula njama kutenda kosa ambapo inadaiwa
kati ya Julai 5, mwaka jana, washitakiwa walikula njama kutenda kosa.
Pia
inadaiwa Julai 5,2015 pembezoni mwa barabara ya Nyerere katika Kituo cha Mafuta
cha Victoria, washitakiwa waliiba gari lenye namba za usajili T 624 CSH aina ya
Eicher mali ya Kampuni ya White Swan.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ ALIYEKUWA USALAMA WA TAIFA AHUKUMIWA MIAKA MIWILI JELA.”
Post a Comment