Tuesday, December 13, 2016
HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA YAINGIA MKATABA KUBORESHA MIUNDOMBINU.
Do you like this story?
Meya wa jiji la Mbeya David Mwashilindi akisaini Mkataba kwa ajili ya uboreshaji wa Miundombinu ya barabara katika jiji la Mbeya.(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
HALMASHAURI
ya Jiji la Mbeya, leo imeingia mkataba na makandarasi mbalimbali wa ujenzi wa
miundombinu ya barabara pamoja na madaraja katika Kata 14.
Mkataba
huo, umesainiwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, David Mwashilindi huku
ukishuhudiwa na baadhi ya madiwani wa Kata husika pamoja na mwanasheria wa
halmashauri hiyo Davis Mbembela.
Awali
akizungumzia tukio hilo kabla ya kusaini, Meya Mwashilindi amesema, mkatba huo,
unalenga kuboresha miundombinu katika baadhi ya kata katika halmashauri
hiyo ambapo kazi hiyo inataraji kuanza mapema mwezi huu.
Aidha,
amesema kuwa mkataba huo unagharimu kiasi cha shilingi milioni 300 na
kwamba kazi kubwa itakayofanyika ni uboreshaji wa barabara na matengenezo ya
madaraja katika kata 14 kati ya 36 zilizomo ndani ya Jiji la Mbeya.
“Kampuni
zilizoingia mkataba leo ni tano na zote ni makandarasi wa ndani na kubwa zaidi
ni wazawa,”amesema.
Pia,
Mwashilindi amewataka makandarasi waliochukua kazi hizo kuhakikisha
wanafanya kazi kwa kiwango kinachotakiwa na kwa muda muafaka huku akiwatoa hofu
juu ya fedha, kwani bajeti ya matengenezo hayo tayari imeidhinishwa..
Hata
hivyo, katika kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa kwa asilimia 100, Mwashilindi
amewataka watendaji pamoja na madiwani kuhakikisha wanatembelea na kukagua
miradi hiyo, wakati ikiendelea kufanyika na kuachana na tabia ya kusubili mradi
ukamilike na kukabidhiwa na ndipo kuanza kubaini kasoro.
“Serikali
imekuwa ikitumia fedha nyingi na asilimia kubwa inatokana na kodi za wananchi
hivyo ninawaombeni madiwani na watumishi hasa wa idara husika kuhakikisha
mnatembelea na kuukagua mradi huu wakati wote wa mchakato, sitapenda kusikia
changamoto mara baada ya mradi kukamilika,”amesema.
Mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA YAINGIA MKATABA KUBORESHA MIUNDOMBINU.”
Post a Comment