Tuesday, December 13, 2016
MWENYEKITI WA CCM, DKT MAGUFULI ATAJA MAMBO 10 ATAKAYOANZA NAYO NDANI YA CCM
Do you like this story?
Leo
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt John Pombe Magufuli ameongoza Kikao
cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) kilichofanyika katika ukumbi wa Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Kikao
hiki kilikuwa ni kikao chake cha kwanza tangu alipokabidhiwa mikoba ya
kukiongoza cha hicho baada ya mwenyekiti aliyekuwepo Dkt Jakaya Mrisho Kikwete
kuomba kung’atuka kabla ya muda wake kuisha.
Akizungumza
na wajumbe wa NEC leo, Dkt Magufuli ametaja mambo 10 ambayo anaanza nayo kama
mwenyekiti wa CCM. Mambo hayo na haya yafuatayo;-
1.
Rushwa
Mwenyekiti
wa CCM Dkt Magufuli alisema kuwa chama hicho ni miongoni mwa taasisi
zinazotuhumiwa sana kwa uwepo wa mianya ya rushwa hasa kipindi cha uchaguzi
ndani ya chama au serikali. Amesema katika kipindi chake cha uongozi
atahakikisha hakuna kiongozi atakayechaguliwa kwa kutoa rushwa.
2.
Uimarishaji wa chama
Jambo
la pili alilosema wakati akizungumza na wajumbe wa NEC zaidi ya 370 alisema
kuwa ni kujenga chama imara kitakachoweza kuwatetea wananchi na kulinda
rasilimali zao. Dkt Magufuli alisema wao wamechaguliwa na wananchi kupitia
chama hivyo hawapaswi kuwa sehemu ya walalamikaji.
3.
Wanachama
Chama
ni wanachama, ndivyo alivyosema akielezea kuwa ni lazima chama kihakikishe
kinaongeza udadi ya wanachama wake hasa vijana. Aidha, ametahadharisha kuwa
wanachama hao wasiwe wananchama hewa, bali wawe ni wanachama wakukitumikia
chama na watakaolipa ada.
4.
Chama kujitegemea kiuchumi
CCM
ina vitega uchumi vingi sana, lakini kila mara tunakuwa ni ombaomba hasa
kipindi cha uchaguzi. Katika kipindi changu cha uongozi hili sitaki kuliona. Ni
lazima tuhakikishe mali za chama zinakinufaisha chama na tuweze kujitegemea
bila kuwa tegemezi kwa mtu yeyote, alisema mwenyekiti Dkt Magufuli.
5.
Wasaliti na makundi
Kumekuwepo
wanachama ambao si waaminifu ndani ya chama, hawa ni hatari ni lazima
tuhakikishe tunakuwa na wanachama wakweli. Pia akizungumzia suala la makundi
Dkt Magufuli alisema kuwa makundi ndani ya chama hasa wakati wa uchaguzi
yamezidi kushamiri, na wengi huendeleza makundi hata baada ya uchaguzi, ni
wakati wa kujenga CCM mmoja.
6.
Chama Imara kuanzia chini
Hapa
alieleza kuwa chama imara ni kile chenye mizizi kuanzia ngazi za chini. Ni
lazima tuwe na chama imara kuanzia ngazi za shina, tawi, kata, wilaya, mkoa
hadi taifa. Hili litafanukiwa kwa sisi tulipo huku juu kushuka hadi chini
katika jitihada za kueleza sera zetu kwa wananchi.
7.
Nafasi za uongozi
Mwenyekiti
wa CCM amesema kuwa wakati wa mtu kuvaa kofia nyingi ndani ya chama ufike
mwisho na kuwa sasa ni wakati wa nafasi moja ya uongozi kushikwa na mtu mmoja.
Akifafanua hili alisema kuwa litasaidia kutoa nafasi kwa watu wengine pia
kukitumikia chama.
8.
Kufutwa vyeo
Akielezea
katiba ya CCM, Dkt Magufuli alisema kuwa katika awamu yake ya uongozi anataka
vyeo ambavyo havujatajwa kwenye katiba ya chama visiwepo. Akitoa mfano wa vyeo
hivyo alisema ni pamoja na Jumuita ya Wazazi, Chipukizi.
9.
Uwajibikaji
Alisema
kuwa chama kina wajibu wa kuwatumikia wanachama wote bila ubaguzi. Alisisitiza
kuwa katika awamu yake ya uongozi hatokubali kuona watu wachache wa vyeo vya
juu wananufaika na chama na mamia ya wanachama wa chini wakiteseka.
10.
Nguvu ya chama
Jambo
hili ambalo alilisema kwa msisitizo na hata kulirudia mara mbilia ni kuwa,
anataka chama kinachoongoza wananchama na si wananchama au mwananchama
anyeongoza chama. Akitilia mkazo hapa alisema mwanachama ndiye anapaswa
kukifuata chama na si chama kumfuata mwanachama au wanachama wachache.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MWENYEKITI WA CCM, DKT MAGUFULI ATAJA MAMBO 10 ATAKAYOANZA NAYO NDANI YA CCM”
Post a Comment