Monday, January 9, 2017
KESI YA MKE WA BILIONEA MSUYA YAJA NA HILI HAPA
Do you like this story?
Maombi ya
kufutiwa mashtaka yaliyowasilishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
jijini hapa na Miriam Msuya, mke wa aliyekuwa bilionea mkubwa jijini Arusha,
Erasto Msuya, leo yamesikilizwa na kutolewa uamuzi mdogo mbele ya hakimu
Mwambapa aliyesema jamhuri ilikuwa na mamlaka ya kuiangalia hati ya mashtaka kabla
haijaenda mahakamani hapo, hivyo jamhuri ikapewa siku mbili kuiangalia upya
hati hiyo na hivyo kupangiwa Januari 11 mwaka huu kuwa siku ya kusikilizwa
tena.
Utetezi huo
uliwasilishwa na wakili wa utetezi, Peter Kibatala, anayemtetea mteja wake,
Miriam Msuya, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya kudaiwa kumuua mdogo wa
marehemu Msuya, Anethe Msuya, Mei 25, mwaka jana, Kigamboni jijini hapa.
Mshitakiwa mwingine katika kesi hiyo ni Revocatus Muyela ambapo kupitia kwa
wakili wao, Kibatala ameiomba mahakama iwafutie mashitaka hayo kwa kuwa hati ya
mashitaka ina mapungufu na haionyeshi kama walikuwa na nia ya kufanya uovu.
Mei 25, mwaka
huu maeneo ya Kibada wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam, Anethe aliuawa
kwa kuchinjwa akiwa nyumbani Kibada. Wauaji hawakuchukua kitu chochote kwenye
nyumba hiyo. Bilionea Msuya aliuawa Agosti, 2015 kwa kupigwa risasi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KESI YA MKE WA BILIONEA MSUYA YAJA NA HILI HAPA”
Post a Comment