Saturday, February 25, 2017
ASKOFU MOKIWA ALONGA,MWENYE USHAHIDI AJITOKEZE
Do you like this story?
Askofu Mkuu wa Dayosidsi ya Dar es salaam wa Kanisa la Anglikani, Dkt
Valentino Mokiwa ambaye yuko kwenye mgogoro na mkuu wake, amehudhuria
misa maalumu ya kuombea amani katika Dayosisi hiyo, huku akisema kuwa
Kanisa hilo limeingiliwa.
Misa hiyo imefanyika katika Usharika wa Mtakatifu Albano ulioko
katikati ya Jiji la Dar es salaam chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la
Polisi.
Ibaada hiyo imefanyika huku kukiwa na mgogoro kati ya Dkt. Mokiwa na
Askofu Mkuu wa Anglikana Dkt. Jacob Chimeledya ambaye alimtaka kiongozi
huyo wa kiroho ajiuzulu kutokana na tuhuma za ubadhirifu.
“Nasema mwenye ushahidi wa chochote ajitokeze, kama mambo ya karatasi
karatasi yanasumbua watu, wezi wanajulikana na mimi nawajua na ushahidi
ninao,”amesema Dkt. Malasusa.
Hata hivyo wakati Ibaada ikiendelea, askari wa Jeshi la Polisi
waliovalia sare walikuwa wakilinda nje ya jengo la Kanisa na
wamewakamata watu wawili wote wanasadikika wanatokea Usharika wa
Magomeni, na kwamba walitaka kuingia kanisani hapo na mabango kuonyesha
kupingana na misa hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ASKOFU MOKIWA ALONGA,MWENYE USHAHIDI AJITOKEZE”
Post a Comment