Friday, February 17, 2017

BIDHAA ZA MILIONI 50 ZATEKETEZWA


Bidhaa zikiteketezwa na TFDA (Picha; Maktaba)

Bidhaa zenye thamani ya shilingi milioni 51 zimeteketezwa baada ya kuingizwa nchini bila kusajiliwa mkoani Mbeya.

Afisa Mfawidhi wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, kitengo cha kuzuia magendo, Ernest Myenda, amesema bidhaa hizo zimeteketezwa baada ya kukamatwa na kubainika kuwa hazijasajiliwa nchini na mamlaka husika, hivyo haziwezi kutozwa kodi kwa mujibu wa sheria.
Amezitaja biadhaa hizo kuwa ni pamoja na vinywaji vikali, maziwa ya watoto, vinywaji baridi na sigara vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 51 imeteketezwa jijini Mbeya baada ya kukamatwa zikiingizwa au kuuzwa nchini kinyume cha sheria.
Mamlaka ya chakula na dawa TFDA, imetoa rai kwa wafanyabiashara nchini kufuata sheria kwa kuuza bidhaa ambazo zimesajiliwa kwa lengo la kulinda afya za watanzania.

0 Responses to “BIDHAA ZA MILIONI 50 ZATEKETEZWA ”

Post a Comment

More to Read