Friday, February 17, 2017
ROBERT HARWARD NAE AKATAA KAZI YA TRUMP YA KUWA MSHAURI WA USALAMA WA TAIFA
Do you like this story?
Mwanajeshi wa
zamani aliyekuwa amependekezwa na Rais wa Marekani Donald Trump kuwa
mshauri wake wa masuala ya usalama wa taifa amekataa kazi hiyo.
Robert Harward alitarajiwa na wengi kuchukua wadhifa huo ulioachwa na Michael Flynn aliyefutwa kazi na Bw Trump Jumatatu.
Afisa
mmoja wa ikulu ya White House alisema sababu ya Bw Harward kukataa
nafasi hizo ni kwamba ana majukumu mengi ya kifamilia na kifedha.
Bw
Flynn alimpotosha makamu wa rais Mike Pence kuhusu mazungumzo yake na
balozi wa Urusi nchini Marekani ambayo aliyafanya kabla yake kuteuliwa
rasmi kuwa mashauri.
Pigo hilo kwa Bw Trump, la kukataliwa kwa
uteuzi wake na Harward, lilitokea saa chache baada ya Bw Trump
kupuuzilia mbali ripoti kwamba utawala wake umekumbwa na mtafaruku
mkubwa.
Alisisitiza kwamba utawala wake unafanya kazi kama "mashine iliyoundwa vyema."
Bw
Harward aliambia shirika la habari la Associated Press kwamba utawala
wa Trump ulikubali sana kuzingatia "mahitaji yangu, ya kitaalamu na
kibinafsi".
"Ni suala la kibinafsi tu," alisema Harward, 60,
ambaye kwa sasa anafanya kazi Abu Dhabi kama afisa mkuu mtendaji wa
kampuni inayofanyia kazi jeshi la Marekani ya Lockheed Martin.
Alipoulizwa
kuhusu taarifa kwamba alikuwa amewasilisha ombi la kutaka aruhusiwe
kuhama na wafanyakazi wake binafsi serikalini, Bw Harward alisema:
"Nafikiri rais ndiye anayefaa kuzungumzia hilo."
Watu wawili wanaopigiwa upatu sana kupewa wadhifa
huo ni Jenerali mstaafu David Petraeus na kaimu mshauri mkuu wa masuala
ya usalamaA wa taifa Keith Kellogg.
Bw Kellogg, ambaye ni jenerali mstaafu wenye nyota tatu, aliteuliwa kuhudumu kama kaimu baada ya Bw Flynn kung'atuka.
Ana
miaka 72 na amehudumu kwa muda mrefu jeshini, ambapo alipigana vita
Vietnam na Iraq kabla ya kustaafu 2003 na kuwa mshauri wa masuala ya
usalama wa kampuni ya programu za kompyuta ya Oracle Corp.
Bw
Petraeus, ni jenerali wa zamani mwenye nyota nne, ambaye alistaafu kama
mkuu wa CIA mwaka 2012 baada ya kubainika kwamba alikabidhi nyaraka
zenye siri kuu kwa mwandishi aliyekuwa akiandika kitabu kuhusu maisha
yake, ambaye alikuwa ameingia kwenye uhusiano nje ya ndoa naye.
Bado anatumikia adhabu ya kuwa chini ya uangalizi kwa miaka miwili kwa kosa la kutomakinika akiwa na nyaraka za siri.
Atahitajika kumfahamisha afisa wa jela anayemfuatilia iwapo atahitaji kuhamia Washington DC.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ROBERT HARWARD NAE AKATAA KAZI YA TRUMP YA KUWA MSHAURI WA USALAMA WA TAIFA”
Post a Comment