Friday, February 17, 2017
VITA DHIDI YA DAWA YA KULEVYA NA UJAMBAZI YAENDELEA MKOANI MBEYA HAYA MAJINA YA WATUHUMIWA KWA MAKOSA MBALIMBALI
Do you like this story?
KUTEKETEZA SHAMBA KUBWA LA BHANGI
Mnamo
tarehe 16.02.2017 majira ya saa 10:20 jioni Jeshi la Polisi Mkoa wa
Mbeya kwa kushirikiana na Kamati Kuu ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Kipolisi
Mbalizi lilifanya Oparesheni ya pamoja katika Kijiji cha Jojo kilichopo Kata ya
Santilya, Tarafa ya Isangati, Wilaya ya Kipolisi Mbalizi, Mkoa wa Mbeya na
kufanikiwa kumkamata UPE NDUTA [30] Mkazi wa Jojo akiwa amelima shamba
la bhangi lenye ukubwa wa ekari moja.
Aidha
katika Oparesheni hiyo zaidi ya miche 2,000
iliyokomaa ilikutwa shambani. Pia nyumbani kwake alikutwa na bhangi kilogram 2 na gram 145. Mtuhumiwa ni mkulima, muuzaji/msafirishaji na mtumiaji wa
dawa za kulevya [Bhangi].
KUPATIKANA NA DAWA ZA KULEVYA [BHANGI].
Mnamo tarehe 11.02.2017 hadi tarehe 16.02.2017
kwa nyakati tofauti, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya misako dhidi ya
watu wanaojihusisha na uuzaji, usafirishaji na matumizi ya dawa za kulevya.
Katika misako hiyo iliyofanyika maeneo
mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya, watuhumiwa wanne walikamatwa wakiwa na dawa
za kulevya aina ya Bhangi misokoto mitatu yenye uzito wa kilogram 15 na gram 685
Watuhumiwa
waliokamatwa wakiwa na dawa za kulevya aina ya Bhangi ni:-
1. GEOFREY ADAMSON [35] Mkazi wa Mabatini
2. ZUBER MWAMBENYA [24] na 3. GWAKISA ANYOSISYE [20]
wote wakazi wa Mama John na
4. PHILIBERT MOSES [35] Mkazi wa Nonde
5. MPOKI IBRAHIM [37] Mkazi wa Kitongoji cha Igogwe
Wilaya ya Rungwe
6. AGUST KIHAULILO @ KIDEVU [63] Mkazi wa Igawa Wilaya ya Mbarali
7. CALVINS MOHAMED [25] Mkazi
wa Ilemi.
8.
NASSORO OMARI [17] Mkazi wa Mwambene
9.
OTHMANI SAIDI [24] Mkazi wa Mwambene
10. KENEDY BROWN
[21] Mkazi wa mwambene
KUPATIKANA NA MALI ZA WIZI.
Tarehe 15.02.2017 na 16.02.2017
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya msako katika maeneo mbalimbali ya Jiji
la Mbeya na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa 11 waliohusika katika kosa la kuvunja Ofisi za Chuo cha Utumishi wa Umma Tawi la Mbeya na kuiba kompyuta 12 ambazo zilikuwa zikitumika kufundisha.
Aidha
katika msako huo vitu mbalimbali vimekamatwa vinavyosadikiwa kuwa vya wizi
pamoja na watuhumiwa ambao kati yao wapo wanaohusika katika matukio ya uvunjaji
na ununuaji wa vitu vya wizi ambao ni:-
1. GABRIEL MMASY [28] Mkazi
wa Uhindini
2. ITIKA KYEJO [Mwanamke] miaka 41 Mkazi
wa Janibichi
3. PETER MWAIPOPO [19] Mkazi
wa Sinde
4. WILLIAM JOSEPH [18] Mkazi
wa Sinde
5. RASHID SHABAN @ CHIDY [30] Mkazi
wa Sinde
6. FRANK CHAULA [25] Mkazi
wa Sokomatola
7. SALVATORY MTEGA [25] Mkazi
wa Sokomatola
8. KEFASY MWAMBENJA [31] Mkazi
wa Kabwe
9. RAPHAEL NGAILO [19] Mkazi
wa Iyunga
10. ABDUL RASHID [44] Mkazi
wa Mbalizi
11. ZAKARIA RASHID KENSE [23] Mlinzi
wa Kampuni ya New Imara Security na Mkazi wa Isanga
Katika msako huo Kompyuta 11 kati ya 12 zilikuwa zimeibiwa katika Chuo cha Utumishi
wa Umma Tawi la Mbeya zimepatikana.
Pia katika upekuzi uliofanyika katika makazi ya
watuhumiwa walipatikana na mali mbalimbali zidhaniwazo za wizi ambazo ni:-
1. Kompyuta
11 na Monitor 01 aina ya HP zilizotambuliwa kuwa ni mali za Chuo cha Utumishi
wa Umma Tawi la Mbeya
2. Monitor
za Kompyuta 16 aina mbalimbali
3. Digital
Camera aina ya Canon
4. Adapter
51 aina mbalimbali
5. Kompyuta
[Desk Top] 37 aina mbalimbali
6. Laptop
10 aina ya HP, IBM, Samsung na Toshiba
7. Mouse
za Kompyuta 07
8. Keyboard
11
9. Kompyuta
aina ya DELL [Working Station] 08
10. Power Supply 23
11. Hard Disk 64
12. DVD ROM 14
13. Lamp
Holder 01
14. Bulb
World Star Lighting pcs 11
15. Spika
moja
16. DVD
Deck mbili aina ya Sony na Singsung
17. Sub
Woofer mbili aina ya Sea Piano na Pintech
18. Stendi
ya TV moja
Watuhumiwa baada ya kuhojiwa walikiri kuhusika
katika matukio ya kuvunja Ofisi Usiku na kuiba pamoja na kununua mali
mbalimbali za wizi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishna wa
Polisi DHAHIRI A. KIDAVASHARI anatoa
wito wa wananchi na wakazi wa Mbeya kufika kituo kikuu cha Polisi Kati kwa
ajili ya utambuzi wa mali zao.
KUPATIKANA NA POMBE MOSHI [GONGO]
Mnamo
kuanzia tarehe 01.02.2017 hadi tarehe 15.02.2017 kwa nyakati tofauti,
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya misako katika maeneo ya Mafiati, Ilomba,
Forest ya Zamani, Itiji, Igogwe, Ngonga na Ikolo Mkoa wa Mbeya na kufanikiwa
kuwakamata watuhumiwa sita wakiwa na
Pombe Moshi [Gongo] yenye jumla ya ujazo
wa lita 39.
Watuhumiwa
waliokamatwa wakiwa na Pombe Moshi ni:-
1. FRANCIS NDEZI [32] Mkazi
wa Forest
2. JAMES KAJANJA [38] Mkazi
wa Forest ya Zamani
3. MATRIDA CHABWELA [49] Mkazi wa Igogwe
4. MOSSES MWAKABENDE [51] Mkazi
wa Ikolo
5. MARTIN MWAMBILYA [45] Mkazi wa Ngonga Wilaya ya Kyela
6. EMANUEL BROWN [21] Mkazi wa Itiji.
7. GEORGE BROWN [57] Mkazi wa Itiji
8.
ITIKA KYEJO [41] Mkazi wa Janibichi
Upelelezi
unaendelea.
KUPATIKANA NA MITAMBO YA KUTENGENEZEA
POMBE MOSHI [GONGO].
Tarehe 16.02.2017 majira ya saa
10:00 asubuhi Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya liliendelea na msako katika
maeneo ya Mtaa wa Kagera, Kata ya Ilomba, Tarafa ya Iyunga, Jiji na Mkoa wa
Mbeya na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja aliyefahamika kwa jina la CLARENCE SUKARI [20] Mkazi wa mtaa wa Kagera akiwa na pombe haramu ya moshi lita 53.
Mtuhumiwa
alikamatwa akiwa na mitambo miwili [mapipa]
ya kutengenezea pombe hiyo. Aidha Pombe hiyo ilikutwa ikiwa imehifadhiwa katika
vidumu 11 vya lita 5. Mtuhumiwa alikiri
kuwa ni mtengenezaji, muuzaji na mtumiaji wa pombe hiyo haramu.
KUPATIKANA NA SILAHA SHORT GUN NA RISASI
ZAKE.
Mnamo tarehe 13.02.2017 majira ya saa
18:02 jioni huko check point ya Igawa,
iliyopo barabara kuu ya Mbeya-Njombe, Tarafa ya Rujewa, Wilaya ya Mbarali, Mkoa
wa Mbeya, Askari Polisi waliokuwa doria eneo hilo walimkamata mtu mmoja aitwaye
NAWAB
HUSSEN [35] Mkazi wa DSM akiwa
na silaha aina ya Short gun (greener marker) yenye namba ya usajili 26515 iliyokuwa imehifadhiwa kwenye
mfuko wa salpheti na risasi mbili ambazo
zilikuwa zimehifadhiwa kwenye mfuko mweusi wa Rambo.
Askari
Polisi waliokuwa doria eneo la Check Point ya Igawa walilitilia shaka Gari
lenye namba za usajili T 289 BWQ Toyota
Hiace na baada ya kufanya upekuzi ndipo walimkuta mtuhumiwa akiwa na silaha
hiyo. Mtuhumiwa alikuwa akisafiri kwa gari hilo kutoka Mbeya kwenda DSM. Gari
hilo ni mali ya Kampuni ya KVD and Supplier LTD inayosambaza magazeti ya NIPASHE na THE GUARDIAN mikoa ya nyanda za juu kusini. Upelelezi unaendelea.
KUKAMATA WATUHUMIWA WA UHALIFU
Mnamo tarehe 04.02.2017 hadi 16.02.2017
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya Misako/Operesheni ya kukamata
watuhumiwa wa matukio mbalimbali ya uhalifu katika maeneo ya Ilemi, Isanga,
Nonde na Airport ya Zamani – Iyela. Katika Operesheni hiyo watuhumiwa wawili
walikamatwa kuhusika katika matukio mbalimbali ya uhalifu ambao ni 1. VICTOR
EBO @ TOLINGA [23] Dereva Bodaboda na 2.
ADAM PHILIMON [21] Dereva Bodaboda, Wote wakazi wa Ilemi Jijini Mbeya.
Katika
upekuzi watuhumiwa hao walikutwa na vifaa mbalimbali ambavyo hutumia katika
matukio ya uhalifu ambavyo ni:-
1.
Mizura [mask]
2.
Shati ya kaki yenye muonekano wa jeshi
3.
Panga moja
4.
Kapelo
5.
Koti
Katika mahojiano na watuhumiwa walikiri kuhusika
katika matukio mbalimbali ya uhalifu ambayo majalada yake ya uchunguzi yalikuwa
tayari yamefunguliwa ambayo ni UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA – PANGA na KUJERUHI.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi DHAHIRI A. KIDAVASHARI anatoa wito kwa wananchi kushirikiana na
Jeshi la Polisi kwa kuwafichua watu na mtandao wa watu wanaojihusisha na
biashara ya dawa za kulevya ili wakamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe
dhidi yao. Aidha Kamanda KIDAVASHARI
anatoa wito kwa wananchi kufanya kazi na kuacha kujihusisha na biashara haramu
ya dawa za kulevya kwani inasababisha kupotea kwa nguvu kazi ya taifa na
kurudisha nyuma maendeleo ya mtu binafsi na taifa kwa ujumla.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “VITA DHIDI YA DAWA YA KULEVYA NA UJAMBAZI YAENDELEA MKOANI MBEYA HAYA MAJINA YA WATUHUMIWA KWA MAKOSA MBALIMBALI ”
Post a Comment