Friday, February 17, 2017
BOSI WA GOOGLE AJIBU BARUA YA MTOTO WA MIAKA ALIYEOMBA KAZI KATIKA KAMPUNI HIYO
Do you like this story?
Kuna watoto wanaopenda kuja kuwa wana anga, zima moto au wapishi watakapokuwa wakubwa – lakini mtoto mmoja nchini Uingereza ameelekeza akili yake yote kwenye moja ya kampuni bora kabisa za teknolojia duniani kwa sasa.
Mtoto huyu, Chloe Bridgewater, ana umri wa
miaka 7, aliandika barua na kuituma kwenye kampuni ya Google akielezea
uwezo wake wa kutumia kompyuta na kueleza pia nia yake ya kuja kufanya
kazi kwenye kampuni hiyo yenye viti vya Maputo (ambavyo hujazwa upepo)
na magari madogo ambayo wafanyakazi wanaendesha wakiwa wanatoka sehemu
moja ya ofisi kwenda nyingine wawapo kazini.
‘Bosi wa Google’, Mkurugenzi Mtendaji
Sundar Pichai, alimjibu mtoto Chloe kwamba ‘anasubiri kupokea’ barua
yake ya maombi ya kazi na kumsisitiza afuate ndoto zake mpaka
zitapotimia.
Chloe anayeishi mji wa Hereford aliamua kuandika barua hiyo baada ya
kuona picha ya ofisi za kampuni ya Google zikiwa zimejaa viti vya kujaza
upepo na magari hayo.
Katika barua aliyoiandika. Chloe
alimwambia Bwana Pichai, ambaye kwenye barua hiyo amemuita jina la ‘Bosi
wa Google’, kwamba anapenda kutumia kompyuta na kucheza ‘game’ kutumia
tablet yake ambayo huutumia kumuongoza roboti.
Pia aliandika kuwa baba yake amemwambia
kwamba akiendelea kuwa mwanafunzi mzuri kama alivyo sasa na akawa
anafaulu shuleni, ipo siku atapata kazi kwenye kampuni ya Google – Chloe
aliongeza kuwa anataka afanye kazi kwenye kiwanda cha kutengeneza
‘chocolate’ na vilevile anapenda kuja kuwa muogelea kwenye mashindano ya
kimataifa ya Olimpiki.
Familia ya bwana Bridgewater ikapokea
barua ya majibu kutoka kwa Mkurugenzi huyo mwanzoni mwa mwezi huu akimpa
moyo mtoto Chloe na kumwambia aendelee kufanyia akazi ndoto zake mpaka
zitakapotimia.
‘Nafurahi kwakuwa unapenda kompyuta na roboti, nategemea utaendelea kujifunza mengi yanayohusu teknolijia,’ ameandika bosi huyo.
‘Bila shaka ukiendelea kufanya kazi kwa
bidii na kufata ndoto zako, utatimiza kila kitu utakachoamua kufanya –
kufanya kazi hapa Google na kuogelea katika mashindano ya Olimpiki.
”Nasubiri kupokea barua yako ya maombi ya kazi utapomaliza masomo yako’.
Andy Bridgewater aliweka kwenye akaunti
yake ya LinkedIn barua hiyo aliyojibiwa na bosi wa Google. Alieleza kuwa
binti yake huyo alipata ajali ya gari miaka michache iliyopita, na
kwamba barua hiyo kutoka Google imemfariji sana binti yake.
‘Baada ya kupata ajali ya gari miaka kadhaa iliyopita, alikuwa hajiamini tena,’ aliandika kwenye akaunti yake ya LinkedIn.
‘Hata hivyo, nikisema kuwa Cloe alifurahi
alipopata barua hii iliyotoka kwa bwana Sundar Pichai mwenyewe itakuwa
sijaelezea vizuri hisia zake.’
‘Sasa anaonekana kuwa na hamu zaidi ya kuhakikisha anafaulu shuleni ili akafanye kazi kwenye kampuni ya Google.’
‘Nashindwa kutoa shukrani zinazostahili
kwa bwana Pichai ambaye yupo bize sana lakini akatenga muda wake kufanya
binti wangu asogee hatua moja mbele kuitimiza ndoto yake, ingawa sina
hakika kama anajua kwamba kuweza kufanya kazi Google ni zaidi ya kukaa
kwenye viti vya kujazwa upepo na kuendesha magari ndani ya ofisi!’
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “BOSI WA GOOGLE AJIBU BARUA YA MTOTO WA MIAKA ALIYEOMBA KAZI KATIKA KAMPUNI HIYO”
Post a Comment