Sunday, February 26, 2017
MAKONDA AELEZA KILICHOMFANYA KUTAJA MAJINA YA WATUHUMIWA WA DAWA ZA KULEVYA
Do you like this story?
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa uamuzi wa
kuwataja hadharani majina ya watuhumiwa wa biashara ya dawa za kulevya ni
kutokana na maombi ya Watanzania waliyayotoa wakati wa serikali ya awamu ya
nne.
Makonda alisema kuwa licha ya watu wengi kupaza sauti zao wakitaka
watuhumiwa wa dawa za kulevya watajwe hadharani, lakini Rais Mstaafu, Dkt
Jakaya Kikwete yeye hakuwataja huku akiacha vyombo husika vifanyekazi zao kwa
usiri.
Lakini kwa upande wa serikali ya awamu ya tano, waliamua kuwataja
watuhumiwa hao ikiwa ni kujibu maombi ya kile watanzania walichokitaka tangu
kipindi cha nyuma, alisema Makonda jana akiwa kwenye semina ya Walimu
Wanaosomesha Quran Tanzania (JUWAQUTA).
“Mzee Jakaya mlimpigia kelele taja, taja, taja, taja, sasa
tulipoingia sisi tukaona wacha tufanye kama alivyokuwa mnataka” alisema RC Makonda.
Aidha, RC Makonda amewakosoa wote walioibuka na kumdhihaki sababu
alitaja majina hayo akisema kuwa giza haliwezi kuondolewa kwa giza bali ni
kuwaleta waliopo gizani kwenye nuru.
“Uliona wapi giza linaondolewa kwa kutumia giza? Aliyefanya
mafichoni anawekwa hadharani na harudii tena,” alisema Makonda.
Katika awamu
ya tatu ya vita dhidi ya dawa za kulevya, RC Makonda hakutangaza majina
hadharani kama alivyofanya katika awamu mbili zilizopita ambapo alimkabidhi
majina 97, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya
Rogers Sianga ili ayashughulikie.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MAKONDA AELEZA KILICHOMFANYA KUTAJA MAJINA YA WATUHUMIWA WA DAWA ZA KULEVYA”
Post a Comment