Friday, February 17, 2017
VITA YA DAWA ZA KULEVYA YAZIDI PAMBA MOTO NCHI NZIMA,KILA MKOA NI KAMATA KAMATA
Do you like this story?
MOTO dhidi ya dawa za kulevya umezidi kusambaa kwa kasi nchini, baada ya watu 247 kukamatwa katika mikoa ya Dodoma na Lindi.
Mkoani Dodoma, watu 168 wamekamatwa na
Jeshi la Polisi katika Wilaya ya Dodoma kwa kukutwa na dawa za kulevya
aina ya bangi, mirungi na cocaine.
Mkuu wa wilaya hiyo, Christina Mndeme, alisema jana kuwa kati ya watuhumiwa hao waliomakatwa, 140 ni wanaume na wanawake ni 28.
Aliwataka viongozi wa ngazi mbalimbali
kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya ikiwa na
pamoja kufanya msako kwenye maeneo yote watakayoyabaini kuna dawa hizo.
Alisema katika Manispaa ya Dodoma maeneo
ambayo yamekuwa kinara kwa matumizi ya dawa hizo ni kata za Makutupora,
Veyula, Msalato, Majengo, Chadulu, Miyuji, Zuzu, Mbabala na Chinangali
West. Zingine ni Madukani, Hazina, Mlezi na Airport.
“Ninawaomba zoezi hili liwe kwa watu wote
na lisiwe l Jeshi la Polisi peke yake, hivyo basi nyinyi wa mitaa vaeni
silaha zote za kuingia kwenye mapambano haya mkizingatia kuwa hapa ni
mkoa ambao upo katikati na ninaamini dawa hizi zinaweza kuwa sehemu ya
njia zinakopitishwa,” alisema Mndeme.
Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Manispaa ya
Dodoma, Matwiga Kyalya, alisema watahakikisha wanashiriki katika vita
dhidi ya dawa za kulevya ambayo ilianzishwa na Rais John Magufuli kwa
maelezo kuwa ni janga la taifa.
Kyalya alisema pamoja na changamoto kubwa
walizonazo wenyeviti hao, lakini watahakikisha wanashiriki katika
kuwabaini wanaojihusisha na dawa hizo ukizingatia kuwa watumiaji wengi
wanaishi kwenye mitaa ambayo wanaiongoza.
Naye, Mkuu wa Polisi Dodoma Mjini, Daniel
Shilah, alisema wapo tayari kupokea taarifa juu ya watu wanaojihusisha
na dawa hizo hata kama wamo askari wake.
79 MBARONI LINDI
Mkoani Lindi, watu 79 walikamatwa kwa tuhuma za makosa mbalimbali, ikiwamo kujihusisha na dawa za kulevya.
Mkoani Lindi, watu 79 walikamatwa kwa tuhuma za makosa mbalimbali, ikiwamo kujihusisha na dawa za kulevya.
Tuhuma nyingine ni uuzaji utengenezaji
gongo, kukutwa noti bandia na silaha katika operesheni maalum ya
kupambana na dawa za kulevya.
Kamanda wa polisi mkoani Lindi, Renatha
Mzinga, alisema jana kuwa watuhumiwa hao walikamatwa katika operesheni
hiyo iliyoanza Januari Mosi 2017 hadi Februari 13 katika wilaya za Lindi
na Kilwa.
Alisema walikamata aina mbali mbali za
dawa za kulevya zikiwamo heroin gramu 50, gongo lita 734, mitambo 14 ya
kutengenezea pombe hiyo, bangi kilo 49 na gramu 987, kete (124), puli 81
na mbegu za bangi gramu 200.
Mzinga alifafanua kuwa watuhumiwa 73
walikamatwa na pombe, mitambo 14 ya kutengenezea gongo, watatu na
bunduki aina ya SMG namba 763529 na magazine mbili zikiwa na risasi
nane. Alieleza kuwa watatu ni raia wa Somalia wanaodaiwa kuingia nchini
kinyume cha sheria.
Aliongeza kuwa walikamata Sh. 25,835,000
na kuwa kati ya hizo Sh. 780,000 zilitolewa na watuhumiwa wakitaka
kuwahonga askari ili wawaachie, na kwamba Sh. 175,000 zilikuwa fedha
bandia.
Pia alisema walikamata Sh. 24,880,000
ambazo zilikuwa kati ya Sh. 70,000,000 zilizoibwa kutoka Chama cha
Ushirika cha Msingi Nahuka Huka Amcos, zilizotakiwa kulipwa kwa
wanachama.
KASI YA KUKAMATA
Kamata kamata imetangazwa pia katika mikoa kadhaa nchini kuhusiana na watuhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya huku wengine wakiendelea kusakwa.
Kamata kamata imetangazwa pia katika mikoa kadhaa nchini kuhusiana na watuhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya huku wengine wakiendelea kusakwa.
Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga limetangaza kwamba limeshawatia mbaroni watu 17 wanaodaiwa kujihusisha na dawa hizo.
Mkoani Iringa, Jeshi hilo limesema
limewatia mbaroni watuhumiwa 21 katika Manispaa ya Iringa, na kwamba
saba wanatuhumiwa kujihusisha na utumiaji wa heroine na wengine 14
wakituhumiwa kujihusisha na utumiaji wa aina nyingine.
Watuhumiwa 47 wametajwa na kutiwa mbaroni
mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya wakati
katika mkoa wa Mwanza mtu mmoja alikamatwa jijini Mwanza Februari 2,
mwaka huu akituhumiwa kukutwa na dawa aina ya heroine pinchi 240 na
ndogo mbili, huku Jeshi la Polisi likisema kuwa linausaka mtandao wote.
Katika Mkoa wa Dar es Salaam ambao
umekuwa kitovu cha vita hiyo iliyochochewa na mkuu wa mkoa huo, Paul
Makonda, orodha ya majina ya watuhumiwa 184 ilikabidhiwa na Makonda
mwenyewe kwa Jeshi la Polisi na kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya
Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga, sambamba na kuwataja baadhi
yao kwa majina.
Orodha ya kwanza ya majina 22 na ya pili
ya majina 65 alizikabidhi kwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar
es Salaam, Kamishna Simon Sirro na ya tatu ya majina 97 alikabidhi kwa
Sianga. Miongoni mwa aliowataja Makonda ni wanasiasa, viongozi wa dini
na wafanyabiashara.
Kwa upande wake, Kamishna Sirro alisema
kuwa jeshi hilo limeshawatia mbaroni watuhumiwa 311 na kwamba baadhi yao
walikutwa wakiwa na vidhibiti vya kete za dawa hizo, akiwamo msanii
Wema Sepetu ambaye ameshafikishwa mahakamani.
Aliongeza kuwa watuhumiwa 100 wanaendelea kusakwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “VITA YA DAWA ZA KULEVYA YAZIDI PAMBA MOTO NCHI NZIMA,KILA MKOA NI KAMATA KAMATA”
Post a Comment