Friday, February 24, 2017

WILAYA YA CHUNYA YAANZA UJENZI WA GEREZA


 
WILAYA ya Chunya mkoani Mbeya imeanza kwa Kasi ujenzi wa kambi ya Gereza la Wilaya litaloondoa adha ya msongamano wa mahabusu katika Gereza la Ruanda jiji Mbeya ambapo husababisha pia ucheleweshwaji  usikilizwaji wa kesi.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa alisema kuwa hivi sasa ujenzi wa Gereza hilo lenye eneo la ekari 165 litakuwa na Nyumba za Askari,mashamba ya kilimo,mifugo na ufundi.
Madusa alisema kuwa hivi sasa shughuli za ujenzi huo zinafadhiliwa na Mdau wa maendeleo Wilayani humo, Merhab Abdullahabu ambaye atakamilisha katika kipindi kisichozidi miezi sita.
Aidha Mkuu wa Wilaya aalisema kuwa kukamilika kwa Gereza hilo kutawaondolea adha wananchi ambao wanakuwa na kesi mahakamani lakini kesi kuchelewa kutokana na mahabusu wao kuhifadhiwa Gereza la Ruanda Mbeya na wakati mwingine Polisi kukosa gari au mafuta ya gari.
Alisema kuwa hali hiyo imekuwa kero kubwa kwa wananchi na wakazi wa Wilaya hiyo hivyo kukamilika kwa Gereza kutasaidia kuondoa msongamano katika Gereza la Ruanda.
Madusa alisema kuwa ujenzi wa gereza hilo wataanza kwanza na zoezi la ufyatuaji wa tofali kwa ajili ya ujenzi wa Gereza ili kuanza kuhifadhi mahabusu.

0 Responses to “WILAYA YA CHUNYA YAANZA UJENZI WA GEREZA ”

Post a Comment

More to Read