Saturday, May 20, 2017
Aliyemuua Samira kwa kumtia karoni apandishwa kizimbani
Do you like this story?
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi limempandisha kizimba cha mahakama ya
Vuga mtuhumiwa Azizi Mbaraka Ali (27) mkaazi wa Meli nne Taveta kwa
tuhuma za kutenda kosa la kuua kwa makusudi.
Imedaiwa
mahakamani hapo na muendesha mashtaka Suleiman Maulid mbele ya hakimu
Isaya Kayange kuwa mtuhumiwa huyo amedaiwa kufanya kosa hilo tarehe 17/6
2015 huko Kiembe samaki Mkoa wa mjini magharibi Unguja ambapo alimuua
Samira Sultani Abdallah jambo ambalo ni kosa kisheria.
Mtuhumiwa hakutakliwa kujibu lolote na amepelekwa rumande hadi tarehe 1/6 mwaka huu kesi yake itakapotajwa tena.
Itakumbukwa kuwa mifupa ya marehemu huyo ilikutwa ndani ya shimo la karo na wazamia lulu mwezi machi mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)